Tetesi za soka Ulaya Jumamosi 04.11.2017

November 5, 2017

 

Hatma ya mkufunzi wa Chelsea Antonio Conte's huenda haijulikani iwapo kikosi chake kitashindwa na klabu ya Manchester United siku ya jumapili.

Conte amethibitisha kuwa mkufunzi wa Chelsea Abramovich alihudhuria kipindi cha mazoezi huku kukiwa na ripoti kwamba bilionea huyo amechoka kumvumilia Conte. (Metro)

 

 

Real Madrid wako tayari kushindana na Barcelona kumsajili kiungo wa kati wa Liverpool na Brazil Phillipe Countinho 24. (Mundo Deportivo - in Spanish)

Mabingwa wa Uhispania Real Madrid wana hamu ya kumsajili kiungo wa kati wa Tottenham Dele Alli, 21. (Marca)

Mkurugenzi wa michezo wa klabu ya Barcelona Robert Fernandez alikuwa akimsaka kiungo wa kati wa Tottenham Christian Eriksen, 25, wakati Spurs ilicheza dhidi ya Real Madrid katika kombe la vilabu bingwa lakini badala yake alifurahishwa na kiungo wa kati ,21, Harry Winks. (Evening Standard)

 

 

 

Mkufunzi wa Manchester City Pep Guardiola hajachoka kutaka kumsajili mshambuliaji wa Arsenal na Chile Alexis Sanchez 28. (Daily Mail)

Kiungo wa kati wa Chelsea na Uhispania Cesc Fabregas, 30, anatarajiwa kuandikisha kandarasi mpya katika uwanja wa Stamford Bridge, na hivyobasi kumaliza uvumi kwamba anaelekea Manchester United. (Evening Standard)

Sunderland wamewasiliana na aliyekuwa mkufunzi wa Middlesbrough Aitor Karanka kuhusu wadhfa wa meneja wa timu hiyo. (Sun)

 

 

 

Winga wa Liverpool Mohamed Salah, 25, anaendelea kuonyesha kwamba ndio mchezaji bora kuwahi kusajiliwa msimu huu kulingana na beki wa zamani wa klabu hiyo Jamie Carragher. (Telegraph)

Mkufunzi wa Burnley Sean Dyche amesisitiza kuwa hakuna mtu aliyezubaishwa na uvumi unaoendelea ambao unamuhusisha na Everton. (Burnley Express)

Mkufunzi wa Leicester Claude Puel anasema kuwa anaweza kumsajili kiungo wa PSG na Ufaransa Hatem ben Arfa mnamo mwezi Januari.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30-alicheza chini ya uongozi wa Puel katika klabu ya Nice 2015-16. (ESPN, via RMC Radio)

Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp anasema kuwa hakuna shinikizo zozote kwa mchezaji Emre Can kusaini kandarasi mpya licha ya kiungo huyo wa Ujerumani kuhusishwa na uhamisho wa Juventus. (Sky Sports)

Juventus itakabiliwa na ushindani mkubwa kutoka kwa klabu ya Manchester City kumsajili Can, huku City ikiwa tayari kumuahidi mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 fursa ya kucheza katikati katika kikosi hicho. (Calciomercato)

Hatma ya kiungo wa kati wa Newcastle Jack Colback na klabu hiyo katika siku za usoni haijulikani huku kocha Rafael Benitez akisema kuwa anaweza kuendelea kufanya mazoezi na kikosi cha wachezaji wasiozidi umri wa miaka 23. (Newcastle Chronicle)

Ajenti wa Edinson Cavani amefichua kwamba mshambuliaji wa Paris St-Germain na Uruguay , 30, yuko tayari kurudi katika klabu yake ya zamani Napoli ya itali.. (sun)

Arsenal haikumsajili kiungo wa kati wa Manchester City david Silva 2005 kwa sababu hawakuamini kwamba angeweza kucheza katika ligi ya Uingereza.

 

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon