Neymar aanza kuimisi Barcelona
Hivi majuzi wikiendi Neymar alionekana nchini Hispania akirudi kuwasalimia washkaji zake wa Barcelona na kuonekana kupiga nao story nyingi sana hii ikiwa karibia mara ya tatu kwa Mbrazil huyo kurudi. Lakini wakati akiwa Hispania kumetoka ripoti toka Ufaransa kwamba Neymar hafurahia tena maisha ya PSG na Ufaransa kwa ujumla na ndio maana kila baada ya mechi huwa anaondoka nchini humo. Ugomvi kati ya Neymar na mshambuliaji mwenzake Edison Cavanni unatajwa kuwa moja kati ya sababu kubwa kwa Neymar kutopapenda PSG huku habari mpya zikidai Neymar hamfurahii kocha wa klabu hiyo. Neymar inasemekana kwamba hafurahii mbinu za kocha Unai Emery na inasemekana kocha huyo hapendwi na wachezaji wengi wa PSG kwani anawafanya wakose raha na kutojisikia amani PSG. Kingine kinachomfanya Neymar kujutia PSG ni habari kwamba wachezaji wenzake hawana furaha kutokana na upendeleo anaopewa na anamiss furaha aliyokuwa nayo akiwa na MSN wakati wa Barcelona.


MZUNGUKO.COM


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu