MWANAUME AFUNGWA JELA MIEZI 6 KWA KUOA MKE WA PILI PAKISTAN. MZUNGUKO.COM
Mahakama nchini Pakistan imemfunga mwanamume mmoja miezi sita jela baada ya kuoa mke wa pili bila idhini kutoka kwa mke wake.

Mahakama hiyo ya mjini Lahore pia ilimuamrisha Shahzad Saqib, kulipa faini ya dola 1,900, na kukataa maoni yake kuwa dini ya kiislamu inamruhusu kuoa hadi wake wanne.

Mke wa kwanza wa Sadiq Ayesha Bibi, alikuwa amefanikiwa kujitetea kuwa kuoa bila idhini yake ulikuwa ni ukiukaji wa sheria za familia nchini Pakistan.

Wanaharakati wa masuala ya wanawake wabasema kuwa kesi hiyo ni pigo kwa ndoa za wake wengi. Pia walisema kuwa itawapa wanawake zaidi walio katika hali kama hizo motisha ya kupeleka kesi mahakamani.

Nchini Pakistan, wanaume wanaotaka kuoa wanawake kadhaa hufanya hivyo baada ya miaka kadhaa na ni lazima wapate idhini kutoka kwa mke wa kwanza.

Baraza la kiislamu nchini Pakistan ambalo hutoa ushauri wa serikali kuhusu masuala ya kiislamu, mara kwa mara limekosoa sheria za familia nchini humo.

Sadiq ana haki ya kukata rufaa kupinga hukumu hiyo ya siku ya Jumatano.


MZUNGUKO.COM


CHANZO: BBC SWAHILITufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu