Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Kabla ya kufunga ndoa hakikisha mmepima haya magonjwa 4 ya kuambukizwa

November 3, 2017

 

 

 

Ndoa ni muungano kati ya mwanamke na mwanamume kuishi pamoja kama mume na mke muda wote wa maisha yao.

Ndoa pia ni zawadi kutoka kwa Mungu mwenye upendo. Kwa hiyo, inatimiza mambo fulani mazuri na inaweza kuleta furaha.  Kwa mfano, ndoa nzuri ndio msingi bora wa maisha ya familia.

 Watoto wanahitaji kulelewa katika mazingira yanayofaa wakiwa na wazazi wanaowapenda, wanaowatia nidhamu, na kuwapa mwongozo.) Hata hivyo, kusudi la ndoa si kupata na kulea watoto tu.

Japo ndoa ni zawadi kutoka kwa Mungu, lakini yatupasa kulinda afya zetu na vizazi vyetu. Je, tutalindaje?  Ili tupate maisha ya furaha siku zote katika maisha yetu ya ndoa na kuondoa migogoro ya kifamilia, ni lazima  kabla ya ndoa tupime maradhi yafuatayo:

  1. Ugonjwa wa kaswende.


Kitaalamu kama syphilis, huu ni ugonjwa hatari sana ambao umeharibu maisha ya watu wengi bila wao kujifahamu. Ugonjwa huu ambao huambukizwa kwa njia ya kujamiana huanza kidogo na kidonda ambacho hakiumi sehemu ambapo wadudu wamepita mfano mdomoni au sehemu za siri.

Kidonda hicho hupona, upele usiowasha hutokea na baadae vyote hivyo hupotea. Ugonjwa huu baadae huingia ndani ya mwili na kuuanza kuharibu viungo vya ndani. Mwisho kabisa ugonjwa huu huahamia kwenye ubongo na kumfanya mtu kuwa kichaa.

2. Ugonjwa wa hepatitis B.


Ugonjwa huu ni hatari na unaua haraka kuliko ukimwi, virusi vya ugonjwa huu huambukizwa kwa njia ya kujamiana na kugusana kwa damu au majimaji ya mwili kama ukimwi lakini ni rahisi zaidi kuambukizwa ugonjwa huu kuliko kupata ukimwi.

Ugonjwa huu hushambulia maini na kuacha makovu, Mgonjwa hupata macho ya njano, homa, maumivu ya kichwa na kadhalika. Ugonjwa huu mwishoni hupelekea kansa ya ini ambayo inaua ndani ya miezi sita.

3. Ugonjwa wa ukimwi.


Huu ni ugonjwa unafahamika kwani unatangazwa sana hasa kwenye vituo vya Radio, Tv, Magazeti na sehemu mbalimbali.

Ugonjwa huu uligundulika karne ya 20 na mpaka sasa umeshaua watu wengi sana na zaidi ya 95% ya wagonjwa waliambukizwa kwa kushiriki ngono bila kinga.

4. Ugonjwa wa gonorea.

 

Huu ni ugonjwa wa zinaa ambao unashambulia jinsia zote yaani Wanaume na Wanawake, mara nyingi Mwanaume hawezi kujificha na ugonjwa huu kwani dalili za ugonjwa huo kama kutoka na usaa kwenye njia ya kukojolea zitamuumbua lakini kwa wananwake ugonjwa huu huweza kukaa kimya na mwanamke hujikuta akisambaza ugonjwa huo bila kujua. Mwishoni ugonjwa huu hushambulia kizazi na kusababisha ugumba.

Licha ya kupima kabla ya ndoa, ni muhimu wanandoa  kutulia na ndoa zao ili kuepuka maradhi yasiyo ya  lazima. Kwani asilimia kubwa ya wanandoa huwa wakishapima kwa mala ya kwanza kabla ya ndoa, basi  hawapimi tehawapimi tena afya zao kwa kuwa wanaaminiana.  Hivo yatupasa kuwa waangalifu katika swala la uaminifu ndani ya ndoa.

Ndoa ni zawadi toka kwa Mungu, lakini ikishaingia maradhi huonekana chungu na wanandoa kuichukia ndoa yao.

 

MZUNGUKO.COM

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload