SAMATTA AMBWAGA MAHREZ TUZO ZA CAF.
Shirikisho la mpira barani africa (CAF)limetoa majina ya wachezaji 30 watakaowania tuzo ya mchezaji bora wa Afrikakwa mwaka 2017.Majina hayo yatapigiwa kura na makocha na manahodha wa timu za taifa na tuzo zitatolewa mwakani mwezi wa januari.


Mchezaji wa kulipwa wa Tanzania Mbwana Ally Samatta ameorodheshwa kwenye list hiyo ya wachezaji hao 30 akiwa kama mchezaji pekee toka Tanzania kufanya hivyo mara ya 2 mfululizo,Mmbwana Samatta anayekipiga katika klabu ya Genk Ubelgij ni nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania TAIFA STARS.

Katika tuzo hizo mchezaji mashuhuri wa Algeria na timu ya Leicester city ya uingereza na aliyekuwa mshindi wa tuzo hiyo mwaka 2016 Riyard Mahrez hajatajwa katika orodha hiyo iliyotolewa na CAF.


Hatua hiyo inatokana na uwezo mdogo wa kuisaidia timu yake katika ligi kuu ya uingereza mpaka sasa tangu walipotwaa ubingwa wa uingereza misimu muiwili iliyopita.

Tunampongeza Mbwana Samatta na tunamtakia kila la heri katika utendaji wa kazi yake.


  • Orodha ya wachezaji wa taji la mchezaji bora Afrika

Vincent Aboubakar (Cameroon & Porto), Karim El Ahmadi (Morocco na Feyenoord), Christian Atsu (Ghana & Newcastle), Pierre-Emerick Aubameyang (Gabon na Borussia Dortmund), Eric Bailly (Cote d'Ivoire na Manchester United), Cedric Bakambu (DR Congo na Villareal), Keita Balde (Senegal & Monaco), Christian Bassogog (Cameroon na Henan Jianye), Yves Bissouma (Mali na Lille), Khalid Boutaib (Morocco na Yeni Malatyaspor), Yacine Brahimi (Algeria na Porto), Essam El Hadary (Egypt na Al Taawoun), Junior Kabananga (DR Congo na Astana), Fackson Kapumbu (Zambia na Zesco), Naby Keita (Guinea na RB Leipzig), Ali Maaloul (Tunisia na Al Ahly), Sadio Mane (Senegal na Liverpool), Moussa Marega (Mali na Porto), Victor Moses (Nigeria na Chelsea), Youssef Msakni (Tunisia na Al Duhail), Michael Olunga (Kenya na Girona), Fabrice Ondoa (Cameroon na Sevilla), Denis Onyango (Uganda na Mamelodi Sundowns), Thomas Partey (Ghana na Atletico Madrid), Mohamed Salah (Egypt na Liverpool), Mbwana Samata (Tanzania na Genk), Jean Michel Seri (Cote d'Ivoire na Nice), Percy Tau (South Africa na Mamelodi Sundowns), Bertrand Traore (Burkina Faso na Lyon), William Troost-Ekong (Nigeria na Bursaspor)


mzunguko.com


Na:Sam Kameme


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu