Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Muuguzi alipwa dola 500,000 katika kisa cha kukataa mgonjwa kutolewa damu.

November 2, 2017

 

Muuguzi mmoja ambaye alikamatwa baada ya kukataa kumruhusu polisi kuchukua sampuli ya damu kutoka kwa mgonjwa ambaye alikuwa amepoteza fahamu amekubali fidia ya dola 500,000.

Alex Wubbels aliafikia makubaliano hayo ya fidia na mji wa Salt Lake na chuu kikuu cha Utah, kwa mujibu wa wakili wake.Kukamatwa kwake na polisi mwezi Julai kulizua ghadhabu baada ya video ya kisahicho kuibuka baadaye. Anaonekana akiwa na pingu mikononi huku akisukumwa na polisi kwenda katika gari.

 

Baadaye aliachiliwa bila ya kushtakiwa. Polisi aliyemkamata alifutwa kazi mwezi uliopita huku mkubwa wake akishushwa madaraka. Polisi Jeff Payne alitumwa kwenda hospitali ya chuo cha Utah tarehe 26 mwezi Julai kuchukua sampuli ya damu kutoka kwa dereva ambaye alikuwa amehusika kwenye ajali ya barabarani na ambaye alikuwa amepoteza fahamu.

Mgonjwa hakuwa ameshukiwa kufanya lolote baya. Bi Wabbels ambaye alikuwa zamu wakati huo alimuambia polisi Payne kuwa hakuwa na waranti wa kuchukua sampuli ya damu jinsi inavyohitajika na sera za hospitali na sheria za jimbo.

Pia alisema kuwa damu haingechukuliwa bila  idhini ya mgonjwa. Bi Wubbels alikataa kumuambia polisi alikokuwa mgonjwa  au kumruhusu kuchukua damu.

Hospitali ya chuo cha Utah baadaye ilisema kwa ilikuwa imeleta sera mpya zinazowazuia polisi kuingia hospitalini wenyeee kuchukua sampuli ya damu.

 

CHANZO: BBC SWAHILI

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload