UMUHIMU WA KITUNGUU SWAUMU KATIKA NDOAHivi karibuni kumekuwapo na tatizo la wanaume wengi kuwahi kufika kileleni, huku kitendo hicho kikichanganywa na sababu mbalimbali ikiwamo mawazo na sababu nyinginezo. Ikiwa wewe unatatizo la kuwahi kufika kileleni basi inasadikika ya kwamba kitunguu swaumu ni tiba tosha. Sifa kuu zinazokifanya kitunguu swaumu kuwa na uwezo na faida nyingi mwilini ni kule kuwa kwake na viasili kadhaa (ingredients) ambavyo vinafanya kazi tofauti tofauti. Uwezo wake wa kiutendaji unatokana na sifa zifuatazo: -Vina uwezo wa kusababisha kutanuka kwa mishipa ya damu (vasodilation) kwa kubadilisha polysulfides zilizopo ndani yake kuwa hydrogen sulfides kwenye seli nyekundu za damu. -Husaidia kuzibiti kiwango cha sukari mwilini kwa kushusha kiwango cha kemikali ya homocystine na hivyo kupunguza madhara ya kisukari. -Ukivikata vipande vidogo vidogo hivi (chop), vitunguu swaumu hutoa kemikali iitwayo kwa kitaalamu kama ‘Allicin’ ambayo ni dawa dhidi ya bakteria, na ‘Phytoncide’ ambayo huua fangasi mbalimbali mwilini.

Jinsi ya kuandaa hicho kitunguu:

1. Chukuwa kitunguu swaumu kimoja. Kigawanyishe katika punje punje 2. chukua punje 6 3. Menya punje moja baada ya nyingine. 4. Kisha vikatekate (chop) vipande vidogo vidogo sana na kisu na uache hivyo katika hewa kwa dakika 10 Baada ya hapo meza kama unavyomeza dawa na maji nusu lita kila unapoenda kulala. Namna nyingine nzuri zaidi ni kuviweka ndani ya kikombe kimoja (robo lita) cha mtindi freshi koroga vizuri na unywe na hii itakusaidia kupunguza harufu mbaya ya kitunguu swaumu huku ukipata faida nyingine mhimu zilizomo kwenye mtindi.


mzunguko.com


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu