JULIO"WAAMUZI HAWATUBEBI”.

October 30, 2017

 

 

Kocha mkuu wa Dodoma Fc Jamhuri Kihwelu ‘Julio’ amesema kuwa licha ya kuwepo kwa lawama kuwa timu yake inabebwa katika ligi daraja la kwanza, ukweli ni kuwa timu yake imejipanga na imeonesha uwezo wa hali ya juu kushinda mechi nyingi

“Kuna watu wanasema sisi tunabebwa, lakini ukiangalia katika mzunguko wa kwanza tumeshinda mechi nyingi tukiwa ugenini. Hiyo ni mbinu za ugenini yaani ‘technical away’ na sio kweli kuwa waamuzi wanatubeba

Julio amesema kuwa timu yake ilijiandaa vizuri kupambana na anamshukuru mungu kwa sababu amefanikisha kufikia malengo yake kama Kocha katika mzunguko wa kwanza baada ya ushindi wake wa 2-1 mbele ya Toto Africans ‘wanakishamapanda’ hiyo jana.

Maneno haya ya Julio yanakuja baada ya mashabiki jijini Mwanza kudai kuwa viongozi wa kiserikali wanataka Dodoma FC ipande ligi kuu ya Tanzania hata kwa mbinu yoyote, hivyo kuamini kuwa timu hiyo itakuwa inabebwa katika michezo yake

Dodoma FC inamaliza mzunguko wa kwanza ikiwa na alama 18. Alama hizi kwa sasa haziwezi kufikiwa na timu yoyote katika kundi hili licha ya Alliance kuwa na mchezo mmoja leo na JKT  Oljoro mkoani Arusha.

 

mzunguko.com

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon