KANE KUWAKOSA MAN U
Mshambuliaji wa Tottenham Harry Kane hatoshiriki katika mechi dhidi ya Man United siku ya Jumamosi baada ya kupata jeraha la goti.

Kane alifunga mabao mawili wakati Spurs ilipoishinda Liverpool 4-1 siku ya Jumapili kabla ya kutolewa katika dakika ya 88.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 ndio mfungaji wa mabao anayeongoza katika ligi ya Uingereza msimu huu akiwa na mabao manane.

''Madaktari na afisa wa matibabu walichukua uamuzi huo wa kutomweka hatarini'' , alisema mkufunzi wa Spurs Mauricio Pochettino.

Hakuna haja ya kufanya hatari na kufanya tatizo kuwa kubwa zaidi.

Kane amefunga mabao 13 katika mechi 12 za mashindano yote msimu huu huku Spurs ikiwa katika nafasi ya 3 katika jedwali la ligi.

Manchester United ni wa pili katika jedwaliwakiwa sawa kwa alama na Spurs.


MZUNGUKO.COM


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu