Gari la mwendo wa kasi zaidi duniani laanza majaribio

Gari lililoundiwa nchini Uingereza linaloweza kukimbia kasi ya kilomita 1,610 kwa saa, linafanyiwa majaribio yake ya kwanza huko Cornwall.

Bloodhound SSC linafanya mikimbio ya mwendo wa chini ya hadi kilomita 320 kwa saa katika uwanja wa ndege wa Newquay.

  • Gari lenye kasi zaidi duniani kujaribiwa Oktoba

Likiendeshwa na Andy Green, gari hilo linalenga kuvunja rekodi ya dunia ya mwendo wa kasi zaidi ardhini.

Jaribio hilo litafanywa kwenye barabara maalum iliyojengwa eneo la Nothern Cape nchini Afrika Kusini.

"Tumeunda gari lisilo la kawaida kabisa, lenye uwezo mkubwa na kasi ya juu zaidi katika historia." Andy Green aliambia BBC.

  • India kujenga treni ya kwanza ya mwendo kasi

Ni miaka 20 tangu mtu aendeshe gari lenye kasi kubwa duniani katika jangwa la Nevada huko Marekani na kuandisha mwendo wa kilomita 1,227 kwa sasa.

Gari hilo jipya limenufaika na teknolojia iliyoboreshwa kwa miongo miwili na litasaidiwa na injini ya ndege ya vita ya Eurofighter-Typhoon ambayo inatumia teknolojia ya roketi.

  • Treni zenye kasi zaidi duniani kuzinduliwa China

Bloodhound inataka kufanya jaribio la kuvunja rekodi ya sasa na kuweka kasi kubwa ambayo hakuna mtu anaweza kuifikia au kuitazama.

Habari kutoka BBC SWAHILI

#GARI #MWENDO #KASI #DUNIA #MAJARIBIO #INDIA #CHINA #MZUNGUKO #OKTOBA

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu