MVUA YAZUA BALAA JIJINI DAR,

October 27, 2017

 

 

 

 

Mvua zilizonyesha usiku wa kuamkia jana jijini Dar es salaam zimeleta maafa makubwa sana katika jiji hili mara baada ya kuripoti kufariki kwa watu kadhaa,kwa habari tulizonazo mpaka sasa kutoka eneo la Mbezi ya Kimara jijini Dar es salaam zinahusisha vifo vya watu 4 katika eneo la  daraja  linalounga Mbezi kibanda cha mkaa(mpakani) na pia eneo hilo ni njia kuu ya mabasi yaendayo mikoani (morogoro road),Taarifa toka kwa mwanahabari wetu zinasema  kwamba majira ya mchana hapo jana Gari ya abiria  aina ya EICHER lilisombwa na maji yaliyokuwa yamejaa darajani hapo na kusababisha vifo hivyo.

 

Mvua hizo zimeleta maafa makubwa katika jiji hili na kusitisha shughuli za maendeleo huku familia nyingi zikibaki bila makazi zimekuwa chanagamoto kubwa kwa siku ya leo oktoba 27 baada ya madaraja na miundombinu kusombwa na maji hivyo kuleta changamoto kubwa ya usafiri.

 

Katika eneo lingine la Mbezi lous kata ya msigani mtaa wa Makonde imetokea shida kubwa ya usafiri mara baada ya maji kumega sehemu ya daraja linalounganisha barabara ya mbezi stand na msigani kuelelekea maeneo ya kwembe,zone na maramba mawili.Aidha mwandishi wetu ameshuhudia wananchi wakilipishwa kiasi cha fedha ili kupita eneo hilo la daraja na vijana kadhaa.

 

mwandishi wetu mpaka anaondoka eneo la tukio ameacha hali ikiwa kama alivyoikuta bila ya chombo chochote cha serukali mahali hapo.Pia katika eneo la kibanda cha mkaa kuna foleni kuna foleni kubwa ya magari  yaendayo mikoani na dalaala pamoja na magari binafsi kufuatia daraja hilo la kibanda cha mkaa kumengwa na maji hivyo magari kupita kwa awamu.

 

Tunaiomba serikali chini ya mkuu wetu wa mkoa Mh Paul Makonda na kamati ya maafa kulifuatilia swala hili kwa ukaribu  ili kutatua changamoto zilizotokea,Pia tunamuomba Mungu aziweke peponi roho za marehemu

AMEN.

 

mzunguko.com

 

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon