MAMBO YANAYOJENGA AU KUBOMOA MAHUSIANO MENGI.


Haya ndugu msomaji karibu tena katika makala yetu pendwa siku ya leo kuhusu kaugonjwa ketu ka moyo, nina uhakika hutatoka bure,kwa kadri za mwenyezi Mungu muweza wa yote muumba wa mbingu na nchi ni vyema kumshukuru yeye kwa maana hakuna lolote linaaloweza kuwa hai bila yeye na hata pumzi tunayovuta mda huu wa sasa ni kwa neema zake yeye mola wetu.Kila wakati ni vyema kuyatafakari matendo yetu kama yanafaa mbele zake baba au la ili tuweze kubadilika na kuwa watu bora zaidi.


Hivi ushawahi kujiuliza ni nini umuhimu wa mapenzi?je ukiyakosa utapata tatizo gani?au kuishi bila mpenzi kuna athari gani kwenye maisha yako?hakika kila mtu hujijibu kilingana na misimamo yake mwenyewe na ndo maana wataaalmu wa mambo hayo wanakwambia usimshauri mtu cha kufanya ila mwelekeze asiingie pabaya.

Kila mahusiano imara kuna sababu nyuma yake,unapoona wapenzi wameaoana kuna mambo mengi ya kufikiria kwani haiko rahisi kama watu wanavyodhania,ukiona wapenzi wako ufukweni mwa bahari wanafurahia sna na kubebana sio kama ni kweli maisha yao ya mapenzi yako hivyo,usiombe uingie wewe utajiona una nuksi aua una mkosi kwani mambo huwa tofauti na ulivyodhania.Ndio ni kweli kwa kuwa uliayatafsiri kwa kuangalia furaha zaidi kuliko uhalisia wa mapenzi yenyewe.


Kama ulikuwa hujui hili ngonjea nikwambie leo,Mapenzi ni mchanganyiko wa maumivu makali na furaha kubwa ya kiasi cha kutoa machozi kwa wakati mmoja,tena ni maumivu makali ya kujuta na kutoa machozi yatakayotiririka siku nzima na moyoni bila kusahaulika vizazi na vizazi.


JE KWA UGUMU WOTE HUO WA MAPENZI NI NINI CHANZO CHA KUDUMISHA MAPENZI?

Hapa ndipo akina dada na akina kaka wengi hufeli na kupigana chini ndani ya kipindi kifupi cha mahusiano yao.kwani kikawaida mahusiano huanza kwa matarajio makubwa sana mbeleni lakini hugeuka na kuwa kiklio kikubwa sana hatimaye na wengine kujia au kuchukua maamuzi ya kuutoa uhai wa mtu.UVUMILIVU.

Hakika hii ni nguzo ya msingi sana katika kudumisha mahusiano ya watu wawili wapendanao,Cha msingi hapa lazima kila mmoja atambue kuwa mnapoanza mahusiano kila mmoja ana tabia yake,hulka zake na misismamo yake,inawezekana huipendi wal kuikubali bali jinsi mnavyokuwa pamoja mnarekebishana taratibu na mwisho wake mnazoeana na kuendana kwa jinsi ambavyo kila mmoja wenu atakuwa tayari kubadilika,ila ukiwa na mtu ambaye hajui shida wala hajui kuvumilia changamoto za kimahusiano na maisha yako au kukubali hali yako na kuivumilia ni dhahiri hamtafika popte,kwani mtashindwana mapema sana.


MSAMAHA.

Neno"NISAMEHE"ni nguzo ya chochote katika ulimwengu,lazima uelewe kwenye Dunia kuna mtu hajawahi kutamka nisamehe mume wangu au nisamehe mke wangu na hakika mahusiano kwako ni mwiba uchomao kwani kila binadamu ana mapungufu yake na kila mmoja anakosea.Usiangalie ukubwa wa kosa agalia je amejutia kosa lake kwa namna gani?na amejishusha kuomba msamaha kwa ukweli au kaamua kukchora tu,lakini neno msamaha kama utatoka moyoni hautaangalia wingi wa makosa wala ukubwa wa kosa neno hili huleta faraja mpya ya upendo na afya."MSAMAHA NI AFYA NA NGUVU YA UPENDO KWA KILA BINADAMU,MSAMAHA NI CHACHU YA KUINUKA NA KUANZA UPYA"rai yangu ni kwamba usiwe mtu wa kukosea mara kwa mara kwani sio kila mtu anaweza kusamehe kila wakati.


HESHIMA.

Mahusiano bila kuheshiamiana ni changamoto nyingine,kumbuka heshima ni tabia ya mtu binafsi japo kuna wakati unaweza kumfundisha mtu,katika mahusiano msipoheshimiana mtaachana mapema sanma kwani kuna wakati msichana atataka kuwa mvulana na kwa mvulana hivyo hivyo,mahusiano yenye heshima huvutia na kudumu kwani kila mmoja hupima anachokiongea kabla ya kukiongea na kufahamu je kinaleta heshima kwa mwenza wake ama la,ukikuta mahusiano hayana heshima ni tatizo kubwa kwani kila mmoja huropoka anachojiskia kwa mwenzake bila kujali eneo,unaposhindwa kumuheshimu mwenza wako hutaona ajabu kunyanyua mkono wako kumpiga au kumtusi,ila heshima iliyotukuka hudumisha mapenzi na yakadumu.


KUAMINIANA NA KUSAIDIANA,

Ni vyema kuaminiana kwenye mahusiano na hasa swala hili linajengwa kwa ukweli wa dhati kwani ukimuamini mwenza wako utampenda na kumwambia ukweli tena kweli tupu,kuaminiana huenda sambamba na kusaidiana,naomba niwe sawia hapa kwenye swala la kusaidiana,kuna wasichana au wavulana kuyafanya mahusiano kama mahala pa kukomoana kwa kupeana majukumu mazito kwa wenza wao na wakishindwa huona kama hawapendwi au hawapo katika mahali sahihi,si kweli:mpenzi wako atakusaidia kadri awezavyo na sio kwa kumkomoa na akiwa hana mpe moyo wa kutafuta zaidi kwani mwisho wa mafanikio yake mtanufaika na kutumia pamoja.


UKWELI.

Ukipata bahati ya kuyapata mahusiano yamejaa ukweli na uhuru wa kweli utafurahi kwa jinsi yanavyodumu,kila binadamu aliiumbwa kusema kweli bali hubadilika kulingana na mazingira yake,ni vyema ukawa mkweli na muwazi kwa mwenza wako pale tatizo litokeapo ili kusaidia mahusiano yako kwani Uongo ni chanzo cha kuvunja mahusiano yako,tafadhali sema ukweli bila kuangalia mpenzi wako ataumia au la kgwa akigundua wewe ni muongo mda sio mrefu atakupiga chini,japo mahusiano mengi yamejengwa kwa uongo ila hayatadumu."UKWELI HUFANYA MAHUSIANO KUWA HURU NA AMANI HUONGEZEKA"Asante ndugu msomaji kwa leo nisikuchoshe kwani kuna makala nzuri sana nimeziandaa kwa ajili yako muda mwingine,hakika utajifunza mengi kwani hili darasa huru la mahusiano,kumbuka sio hayo tu yapo mengi sana ambayo ni msingi mkubwa wa mahusiano.


USHAURI:USIKUBALI KUINGIA KWENYE MAHUSIANO NA MTU AMBAYE UNAFAHAMU HAUNA HISIA NAE NI BORA KUMWAMBIA UKWELI IKO SIKU ATAYAPATA MAPEZNI YAKE KULIKO KUMDANGANYA KUJA KUMUUMIZA BADAE,LAANA YAKE ITAYATAFUNA MAISHA YAKO DAIMA."


NA.MWAL.KAMEME


mzunguko.comTufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu