Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

FAHAMU TIMU GANI ITAIBUKA BINGWA JUMAMOSI WATANI WA JADI.

October 25, 2017

 

 

Jumamosi oktoba 28 utashuhudiwa mchezo kati ya timu mbili kongwe nchini Tanzania,hiyo itakuwa mechi ya mzunguko wa kwanza wa ligi kuu Tanzania bara msimu wa 2017/18.Mechi hiyo itapigwa majira ya saa 10:00jion kwa masaa ya Africa mashariki viingilio vishatangazwa na Shirikisho la mpira Tanzania(TFF) tangu juma lililopita mwishon huku VIP ikiwa ni sh 20000 na mzunguko kawaida ni shilingi 10000.

 

Utamu wa mechi ya watani wa jadi hutoka kwa mashabiki wa timu hizo zinazopendwa zaid Tanzania huku Yanga akiwa bingwa mtetezi wa ligi kuu mara tatu mfululizo na Simba akiwa hajalinusa kombe tangu mwaka 2012 alipolibeba kwa mara ya mwisho.

Mechi ya mwisho ya watani wa jadi iliisha kwa Simba kubeba ngao ya hisani kwa ushindi wa matuta  uliopigwa uwanja wa Taifa,ulikuwa mchezo mtamu na wa kusisimua sana kwani mpaka dakika  ya 90 hakuna timu iliyokuwa imeona lango la mwenzake.

 

 Mechi ya jumamosi lazima kila timu ifanye kazi ya ziada sana ili kupata ushindi kwani timu zote msimu huu  ni ngumu na maandalizi ni ya kutosha kwa kila timu.

 

JE NANI ATAIBUKA MSHINDI?

1:SIMBA.

kwanini?

UPANA WA KIKOSI.

Hapo ndipo ugumu unapokuja kwani timu zote zimepata muda wa wiki mioja kujiandaa na mtanange huo wa kihistoria,Simba ana nafasi kubwa ya kuibuka mshindi katika mechi hiyo kwan ana kikosi kipana sana tofauti na wenzao Yanga wenye kikosi kidogo kuliko simba,Timu ya simba akitoka fundi anaingia fundi mwingine kwani katika kila namba simba ina wachezaji nyota zaidi ya wawili.

 

MWANZO MZURI WA LIGI:

Hilo halina ubishi kwani timu ya simba imeanza vizuri tofauti na timu nyingine ya ligi kuu ya Tanzania bara,Simba imeshinda zaidi ya magoli 15 mpaka sasa huku wapinzani wakichezea zaid ya goli 3 kwa mechi kadhaa mfululizo na kuifanya timu ya kuogopwa zaidi msimu huu.Mpaka sasa Simba iko kileleni mwa ligi kuu Tanzania bara.

 

SIMBA INA HAMASA  KUBWA ZAIDI.

Timu ya simba iko vizuri sana kwa upande wa hamasa tofauti ya Yanga mpaka muda huu,Yanga imekutana na maswahibu mengi tofauti na Yanga kwani  wiki kadhaa nyumba wachezaji wameshawahi kugoma kisa kulipwa mishahara yao ya miezi kadhaa hivyo kuwa na mgogoro kiasi fulani hasa baada ya mwenyekiti wao kupata matatizo kidogo na kuifanya timu kuyumba kiasi fulani.

 

AINA YA WACHEZAJI.

Simba ina wachezaji wenye uwezo mkubwa zaidi na wana uwezo wa kubadili matokeo kwa mda wowote wa mechi ikiwa inaendelea,mfano washambuliaji wake Emanuel OKWI,amekuwa tishio sana  katika ligio msimu huu kwani anaongoza kwa magoli,ana magoli 8 mpaka sasa na ameshafunga magoli 4 katika mechi moja  na kuwa mshambuliaji hatari zaidi,Mohamedi ibrahimu Mo nae ni tishio san kwa mechi ya jumamosi  bila kumsahau  Kichuya ambaye ni tishio kubwa.

 

KUJIAMINI.

Simba imekuwa timu ya kwanza msimu huu kuanza vyema sana tofauti na Mtibwa ambayo nayo  si haba i,ila Simba wamejengewa kujiamini sana kwa msimu huu kwani wana kila aina ya wachezaji wanaoweza kufanya chochote ndani ya uwanja.hiyo yaweza kuwa sababu kubwa ya ushindi wa timu hiyo jumamosi.

 

2:YANGA.

Mpaka sasa wanalingana na Simba kwa alama ila magoli ndo toafuti kubwa, kwani simba ina magoli mengi zaidi ya 15 mpaka sasa kwa wakati huu wa mzunguko wa kwanza.Yanga wameanza kusua sua sana kwenye ligi  ila wamejitahidi kupanda na kufanya vizuri  mpaka mechi ya mwisho waliposhinda 4-0 kama wenzao simba.

 

WACHEZAJI WA KIPEKEE.

Yanga imekuwa na wachezaji wa kipekee sana msimu huu wengine wakiwa hawana majina kama wa Simba,hii inatokana na wachezaji wake nyota kuhama timu hiyo msimu uliopita kama Simon Msuva na Haruna Niyonzima,wachezaji kama Buswita,Mwashiuya,Ibrahimu Ajibu alietokea Simba na kuwa tishio zaidi kwa timu ya Yanga msimu huu kwani ameipa yanga jumla ya alama 12 mpaka sasa.

 

 

KUDHARAULIWA.

Hakika hii inaonekana kabisa  kwani timu ya Yanga msimu huu inaonekana si lolote si chochote baada ya misimu mitatu ya ligi kuwa mizuri na ya mafanikio,hivyo ili kuonyesha sio wateja na wazuri lazima waonyeshe umwamba wao kwa Simba na hivyo hawatakubali kufungwa na kuifanya mechi kuwa ngumu sana na inawezekana wakashinda mechi hiyo kwani simba wanajiamini sana na hilo linaweza kuawaathiri sana.

 

KIKOSI KIDOGO NA KIZURI SANA.

Yanga wana kikosi kizuri sana japokuwa ni kidogo sana kwani mpaka  sasa wako nafasi ya pili ya ligi kuu huku wakilingana alama na  timu ilyoko kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ya Tanzania bara.hakika kikosi hiki cha Yanga kinaweza kufanya makubwa sana katika mechi ya jumamosi.

 

Mechi ya juamamosi itakuwa na msisimko sana kwa kuwa  Simba na Yanga msimu huu ziko kama zina kiwango kinachofanana na ndo maana mpaka leo alama katika msimamo wa ligi zinafanana na kutofautishwa na magoli,Sioni mshindi wa moja kwa moja katika mechi hiyo ila naamini kila timu ina nafasi ya kupata ubingwa msimu na katika mechi ya ijumaa kila timu ina nafasi ya kushinda katika mechi hiyo ya jumamosi.

 

 

Mzunguko.com

 

Na:Sam Kameme.

 

 

 

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload