Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

JIMBO LA KATALUNYA BADO HALI NI TETEE

October 25, 2017

 

Jimbo la Catalonia nchini Uhispania linapanga kukata rufaa katika mahakama ya katiba, kupinga kutumika kwa kifungu cha 155 ambacho kitatoa ruhusa kwa Serikali Kuu ya Uhispania kuchukua mamlaka ya kulitawala moja kwa moja jimbo hilo. Hayo yameelezwa leo na msemaji wa jimbo hilo, Jordi Turull. Siku ya Ijumaa, baraza la seneti la Uhispania linatarajiwa kuidhinisha serikali kutumia mamlaka yake maalum. Wakati huo huo, chama cha CUP kinachounga mkono Catalonia kujitenga na Uhispania, kimesema serikali ya Catalonia inafikiria kuitisha uchaguzi wa mapema. Hata hivyo, mwanasiasa wa chama hicho, Carles Riera amesema leo kuwa chama chake kinachofuata siasa za mrengo mkali wa kushoto, kitapinga hatua kama hiyo. Riera amesema uchaguzi wa jimbo hilo ni silaha ya kuifuta kura ya maoni ya Oktoba Mosi na matakwa ya wananchi wengi wa Catalonia.

 

mzunguko.com

CHANZO:BBC

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload