HIZI NDIZO SABABU ZINAZOPELEKEA WAPENZI KUACHANA, Kuwa makini kwa mambo yafuatayo.

October 25, 2017

 

 

Ukiwa katika mahusiano usiwe mtu wa kuangalia mambo kwa juu juu basi kila kitu kwako kitakua kigumu.kusoma unaweza kuona ni kugumu,kufanya kazi kugumu, hata kusubiri mshahara unaweza kuona  ni kugumu

Urahisi kwako unaweza kuwa katika kutumia pesa,pengine na kula tu.Ila watu waelevu kwako  kila kitu kinaweza kuwa tufauti na wewe.

 

1.Unachoona kigumu kwao wanahisi  si ugumu  bali ni changamoto za kuzidisha jitihada na umakini tu.kwenye mapenzi pia hali haiku tofauti  sana  wale wanao achana kila siku kama ndivyo wanakosewa sana kuliko wale ambao hawaachani,hapana.suala ni lilelile tu.

 

2.Wakati mwingine wakiona tufauti  zao ni kama changamoto za kusomana tabia na kuamua  kuishi kutokana na kila mmoja kua na maisha yake.suala la uvumilivu kwao hamna

 

3.Hakuna mapenzi  duniani  yanayoweza kushamiri  bila suala hili.usipokua na moyo wa uvumilivu katika mapenzi basi kila mtuwa kuanzisha mahusiano mapya.hayo si maisha sasa

 

4.Mahusiano  yaliyodumu si kwa kua wahusika hawakoseani  au makosa wanayokoseana ni madogo sana.Hapana kila binadamu ana mapungufu yake.Wote huwa wanakoseana ila tofauti yake  na wengine ni kwamba busara na uvumilivu  huwa msingi wa mapenzi  yao na ndiyo maana tunaona  binadamu mpaka leo.

 

5.Ni binadam gani unaweza kuishi nae na msikosane?Ni  nani  mwenye uwezo wa kukupa  unachotaka kila siku? Hakuna binadamu wa haina hiyo.

 

6.Hivyo unavotaka kuachana na uliyenae suala la kujiuliza ni kua mara ngapi  umemueleza kuhusiana  na suala unalotaka kumuachia .Na hiyo isitoshe tu pia jiulize ni sababu gani inayomfanya kutenda suala ilo.Ukimaliza hapo rudi nyuma na jiulize tena huwa unatumia maneno  ya aina gani katika kumkanya.

 

7.Maana wengine baada ya kukosewa wao huwa hawawakanyi vyema weza wao bali huripuka  kwa maneno  makali na dharau.Matokeo yake sasa wahusika baada ya kuwasikiliza na kufanyia kazi maneno  wanayo ambiwa  kutokana na makosa yao ,wao huwapuuzia na kuwaona wasema ovyo.

 

8.Ndivyo,kukosewa kunaumiza sana ila jiulize ni kitu gani  kimetokea bila sababu? Kwenye makosa ya mpenzi kwako kuna  sababu nyuma yake,hebu itafute badala ya kulalamika.

 

9.Mapenzi yasiokua na uvumilivu ndani yake hayana maisha marefu kwa sababu binadam ni kiumbe mwenye kukosea.

 

10.Mpenzi wako ni furaha yako kwa maana ndie mtu ulieridhia nae kuwa nae katika masuala nyeti yahusuyo maisha yako.Sasa kwa nini uwe tayari kumpoteza kisa kachelewa kurudi.

 

11.Kwa kua huyo ulie naye unampenda kwa dhati basi amua kwenda nae taratibu ukijitaidi kumbadilisha tabia zake.Usiogope,inawezekana suala ni uvumilivu  na kujiamini tu.Kukubali kumpoteza unayempenda kwa kukosa uvumilivu ni kujitakia kuingia katika maisha ya kutanga tanga tu.

 

 

mzunguko.com

Kumbuka wanaovumilia siku zote ndo huwa wanabaki na ushindi.Bila uvumilivu Mandela asingekuja kuwa Raisi wa. siku Afrika kusini Uvumilivu ni kila kitu katika maisha zote

BY BERNADETA NJEWIKE.

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon