NIYONZIMA YUKO GADO 100%SIMBA IKIVAANA NA YANGA OKTOBA 28.


KIUNGO nyota wa Simba inayodhaminiwa na Kampuni ya kubashiri Matokeo Michezo ya SportPesa, Mnyarwanda Haruna Niyonzima, amesema mashabiki wa timu hiyo wajiandae kumuoana Niyonzima Mpya baada ya muda mfupi.


Akizungumza jijini Dar es salaam, Niyonzima lisema kuwa mashabiki wengi wamekuwa wakihoji kiwango chake cha sasa na wengi wakiona kama hayupo kwenye kiwango chake kinachofahamika.

“ Mashabiki wawe wavumilivu, inawezekana sijawa kwenye kiwango walichokizoea, lakini wakumbuke nilikosa sehemu ya maandalizi kwa ajili ya msimu mpya ( Pre Season)”, alisema Niyonzima.


Aliongeza kuwa kwa sasa amekuwa kwenye program maalum aliyopewa na Kocha wa timu hiyo ili kurejea kwenye makali yake na anaamini wiki mbili zijazo atakuwa kwenye ubora wake.

“ Kwa wale wanaojua mpira wanafahamu nazungumza nini na hawawezi kunilaumu, ligi bado mbichi hata michezo 10 hatujafikisha, naamini baada ya muda nitarejea kwenye makali waliyoyazoea,” alisema Niyonzima.


Aidha , aliendelea kuwa Ligi msimu huu ni ngumu na yenye ushindani mkubwa na hiyo ni kutokana na timu kujiandaa vyema.

“ Nafikiria na kingine ni kuanza kuja wadhamini kwa wingi kwenye klabu mbali mbali kumeongeza ushindani, tulizoea kuona Klabu zaSimba Yanga na Azam kuwa na wadhamini, lakini kwa sasa unaweza kuona wadhamini wanajitokeza kwa timu nyingine kama Singida United, Mbao na nyingine,” alimalizia kwa kusema hayo.


mzunguko.com


By Mwanahamis Mkali


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu