HAYA NI BAADHI YA MAMBO AMBAYO MWANAMKE HAWEZI KU YAWEKA WAZI KATIKA MAHUSIANO.


Unapoanzisha mahusianona mwanamke yoyote yale faham fikayapo baadhi ya vitu hawezi kukwambia na baadhii ya mambo hayo ni


1.Idadi ya wapenzi wake wa zamani

Wanaume wengi hupenda kujua wao ni wa ngapi kua na mwanamke Fulani.Lakini mwanamke hawezi akamwambia wewe ni wa n gap.kumuuliza jambo hili kunamkera sana mwanamke na ndio maana mara nyingi hawezi akakwambia ukweli.


2. Anakulinganisha na mpenzi wa zamani

Mwanamke mara nyingi anakulinganisha na mpenzi wake wa zamani japokua hawezi kukwambia waziwazi.wakati mwingine wanawake kuwatamani wapenzi wao wa zamani na hata kurudiana nao wakikosa mtu aliye bora kuliko mpenzi wake wa zamani.


3.Kasoro zako

Mwanamke kamwe hawezi kukwambia kasoro zako.Wanawake wanajua kumfichia mpenzi wao mambo wasiotaka yajulikane kwa wengine na kwa mpenzi wake.Wanajua njia za kiujanja za kutumia ili kufichua siri zako zote.Mwanamke hawezi kukwambia kasoro zako kwa kuogopa kukuumiza.


4.Mapungufu yake

Mwanamke hawezi kukwambia mapungufu yake ladba kwa kuhofia kushushwa thamani.Wanawake ni wasiri sana kwa mapungufu yao wanajua vyema hofu zinazo muandama,vitu vinavyowakosesha usingizi na mambo yanayowaelemea.maishani japo sio rahisi kuonyesha.Kwa nje anaweza akaonekana yuko vizuri na hana tatizo kumbe ndani ana matatizo au mapungufu.Anaweza kufanya yote kufunika upungufu wake


5. Huwa unampagawisha mpaka anakosa la kusema.

Hili halisemi kabisa mwanamke kwa sababu anaona haya kutumi maneno ya wazi kueleza raha anayopata.Maneno ya kuzuzua ni himaya ya mwanaume ,lakini wakati mwingine wapo wasioweza kuficha.


6. Haumridhishi katika tendo la ndoa.

Wanawake wengi hawapendi kusema hawaridhiki kwenye tendo la ndoa.Wanawake wanahitaji kuandaliwakwa dakika 10,20 ama nusu saa. Mara nyingine wanaume huwai kabla mwanamke hajawa tayari na hivyo kushindwa kuridhika lakini hawezi kusema

Hayo ni baadhi ya mambo ambayo wanawake wengi hawawezi kuyaweka wazi kaika mahusiano yake pale anapoanzisha mahusiano


mzunguko.com


BY BERNADETA NJEWIKE


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu