Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

RONALDO ABEBA TUZO MWANASOKA BORA WA FIFA KWA MARA NYINGINE,GIROUD,MBAPE NAO WANG'AA

October 23, 2017

 

 

Baada ya kuchukua tuzo ya mwanasoka bora wa kiume wa  FIFA 2016 Christiano Ronaldo(Mnyama CR7)ameendelea kumtesa mpinzani wake wa karibu Lionel Messi kwa mwaka wa pili mfululizo  baada ya kuinyakua na tuzo ya mwaka huu ya mchezaji bora wa dunia wa FIFA,

 

Tuzo zilitolewa jijini London  akikabithiwa na Diego Maradonna  pamoja na Ronaldo De Lima, Ronaldo amepata kura nyingi zaidi ya mastaa wenzake waliokuwa wanachuana katika tuzo hizo Lionel Messi na Neymar,

Christiano ronaldo ameiwezesha klabu yake ya Real Madrid kubeba mataji muhimu msimu uliopita kama UEFA,Ligi ya Hispania na UEFA super cup,huku Neymar na Messi wakiisadia Barca kubeba kikombea cha kombe la mfalme,

 

Tuzo hizo zilianza kutolewa tena baada ya kutenganishwa na tuzo za Mchezaji bora wa Dunia (ballon dor) zitolewazo na waandishi pamoja na FIFA,hivyo mwaka jna na mwaka huu tuzo hizo kutenganishwa na kufanya kila koja kutolewa kivyake.

Hii inakuwa mara ya pili kwa mreno huyo kubeba tuzo hiyo tangu zitenganishwe hapo mwaka jana alipoibeba.

Mbali na tuzo hiyo wachezaji wengine waliopata tuzo hizo ni Olivier Giroud wa Arsenal(goli la mwaka) na Kylian Mbappe aliyechuku tuzo ya mchezaji kinda aliyeng'ara zaid akiwa na Monaco kabla ya kwenda PSG kwa mkopo msimu huu.

kocha wa Real madrid Zinedine Zidane amechukua kocha bora wa mwaka wa FIFA 2017.Kipa bora imebebwa na Gianlugi Buffon,

Kikosi bora cha FIFA cha dunia Golikipa  Buffon,Marcelo,dan alves,Bonucci,Luke modric,iniesta,Ton Kroos,Messi,Neymar na Ronaldo.

 

 

mzunguko.com

 

Na:Sam Kameme

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload