Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

PROF UDSM AUKWAA UGAVANA WA BENKI KUU.

October 24, 2017

 

 

Raisi wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh.Dr John Pombe Magufuli ameendelea kuwatumia wasomi mbalimbali katika serikali  yake baada ya jana kumteua Prof Florence Luoga Kutoka Chuo kikuu Dar es salaam(UDSM).Huo unakuwa mwendelezo wa wa Muheshimiwa Raisi kuteuwa wasomi katika nynja mbalimbali hasa nyeti kutoka chuo hicho kama alivyafanya kwa Prof Paramagamba Kabudi na wengine wengi aliowateua toka chuoni hapo.

 

Profesa Luoga aliteuliwa hiyo jana katika tafrija hiyo iliyofanyikia ikulu Dar es salaam ikiudhuriwa na watu mabalimbali wa nyanja tofauti ikiwemo vyama vya upinzani,Prof Luoga anachukua nafasi ya Profesa  Benno Ndulu anayemaliza muda wake Januari 17 mwakani'

 

Muheshiwa Raisi amemteua Profesa Luoga kwani ni mtaalamu wa maswala ya sheria za kodi na alikuwa mkufunzi katika chuo kikuu cha Dar es salaam kutoka kitivo cha sheria(UNIVERSITY OF DAR ES SALAAM SCHOOL OF LAW   UDsol) na ametumikia chuo kikuu cha Dar es salaam kama Makamu mkuu wa chuo upande wa taaluma (DVC ACADEMIC).

 

Muheshimiwa Magufuli amesema kwamba Prof Benno amefanya kazi kubwa sana ya kuinua uchumi na kupunguza mfumuko wa bei lakini pia amesema prof Luoga atakuwa mtu sahihi katika kutatua changamoto za matatizo ya upotevu wa fedha za serikali has kwa upande wa fedha za nje na ukwepaji wa kodi.

 

Kampuni nzima ya Generation Work inampongeza Pfof Luoga kwa uteuzi huo na inamuombea kazi njema ya ufanisi mkubwa ili kusogeza mbele taifa letu kiuchumi  na kila nyanja,kwani Prof Luoga ni mtu sahihi kabisa wa kazi hiyo na mtu makini katika utendaji kwani ni mmojawapo wawajumbe wa kamati  iliyoundwa na Raisi katika uchunguzi wa suala la makinia na kuleta ripoti iliyozaa matunda makubwa.

 

mzunguko.com

 

Na:Sam  Kameme

 

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload