Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

MHESHIMIWA MAKONDA AWATOA HOFU WAKAZI WAKE.

October 24, 2017

 

 

 

 

 

 

Mkuu  wa mkoa wa Dar es salaam Mh.Paul Makonda  amewatoa hofu wananachi wake kufuatia  taarifa ya kubomolewa nyumba kwa wakazi ambao wamevamia maeneo na kujenga pasipo vibali,pia kwa waliojenga nyumba zisizo na hati maliki lilitolewa kutoka wizara ya adrhi nyumba na maendeleo ya makazi kupitia kwa Waziri wake William Lukuvi akiwaagiza Wakurugenzi wa Halmashauri,maafisa ardhi kuwekea alama X nyumba zote zilizojengwa maeneo ya dhuluma.

 

Taarifa hiyo ilitolewa tarehe 23 oktoba na vyombo vya habari Mheshimiwa Lukuvi akikaririwa akitoa agizo hilo,Pia Waziri Lukuvi alitoa ufafanuzi na kusema wale waliojenga katika maeneo ya dhuluma  na kutumia nguvu kuchukua viwanja vya watu wengine  sheria itafata mkondo wake,hivyo waziri alitoa wito kwa wananchi wote kurasimisha makazi yao kwa faida yao na taifa kwa ujumla.

 

Akiliongelea swala hilo mheshimiwa mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Bw Paul Mkonda ametolea ufafanuzi katika mitandao ya kijamii na kusema kwamba serikali inarasimisha makazi akiwataka wananchi wenye mpango wa kujenga kufuata utaratibu toka wizara ya ardhi ili kuepuka usmbufu wa kubomolewa hapo badae,pia amesema kama ilivyofanyika kimara ambapo hati zaidi ya  6000 zimetolewa kwa waliojenga katika makazi yasiyo rasmi vivyo hivyo itakuwa sawa na itakavyofanyika tarehe 27 oktoba Makongo Juu,pia mheshimiwa Makonda amesema kuna changamoto ya upatikanaji wa vibali vya ujenzi na hivyo isiwe adhabu kwa wananchi wanaotaka kujenga

Pia ametaja changamoto nyingi ambazo hufanya wananchi kushindwa kufata vibali na hivyo kutengeza mianya ya rushwa katika nyanja hiyo ya ujenzi.

 

mzunguko.com

 

Na:Sam Kameme

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload