Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

ELEWA MADHARA YA POMBE KWA BINADAMU.

October 24, 2017

 

 

 

POMBE NI NINI?

Pombe ni mjumuisho waaina zote  za vilevi unazozifahamu, zipo pombe za aina mbali mbali na huwa zinatengenezwa na kutumika katika jamii zote duniani,  japo kuna  baadhi ya dini haziruhusu pombe. Tukiangalia historia ya pombe  inaonesha tangu zamani sana ilikuwepo.

Japo pombe ni kinywaji kinachopendwa zaidi, tuangaie kiwango sahihi cha pombe kinachotakiwa  katika jamii.

 

 

 

 

Kitaalamu mwanaume mmoja anatakiwa anywe vinywaji viwili vya pombe, wakati huo mwanamke anatakia anywe kinywaji kimoja cha pombe. Ninaposema kinywaji simaanishi chupa ya pombe ila namaaanisha kiasi cha pombe na asilimia zake ndani.  Kw mfano:- Milimita 354 za bia ya kawaida yenye 5% ndio kinywaji kimoja, Milimita 147 za Wine au mvinyo yenye 12% ndio kinywaji kimoja na Milimita 44 za pombe kali Viroba zenye 40% ndio kinywaji kimoja. Tukiangalia kwa wastani mwanaume anapaswa kunywa bia mbili kwa siku huku mwanamke anatakiwa kunywa  bia moja kwa siku.

Athari za matumizi ya muda mrefu ya pombe.

 

1.Hutapakaa baina ya uwezekano wa faida za kiafya kwa watumiaji wa viwango vya chini  vya pombe hadi madhara makubwa katika hali ya MATUMIZI MABAYA YA POMBE kwa muda  mrefu. Viwango  vya juu vya mtumizi ya pombe huhusiana na ongezeko la hatari ya kuendeleza ulevi, ugonjwa wa moyo, kutofyonza vyakula, ugonjwa sugu wa Kongosho, uginjwa wa Ini na Kansa. Uharibifu kwa mfumo  wa neva za pembeni unaweza kusababishwa  na matumizi ya kila mara ya pombe.

 

 

 

 

2. upo uwezekano wa kuharibu takribani kila kiungo na mfumo katika mwili.

 

3.  Inakuweka mbali na familia yako, kwa kuwa muda mwingi unakuwa Baa na watu wengine.

 

4. Inachangia ongezeko la Zinaa na Ngono  zembe.a

 

5.Upungufu wa ngvu za kiume.

 

6. Kichaa cha pombe( Mtu hawezi  kufanya kazi bila ya pombe, au anakuwa kama mgonjwa lakini akipewa  pombe anakuwa mzima).

 

7. Kuongeza kasi kwa baadhi ya magonjwa hata kama unatumia dawa, kama vile Kifua kikuu,Kansa,Kisukari, Shinikizo la damu la kupanda. N.k

 

8. Kukosa hamu ya kula( Anorexia) .

 

HAYA NI BAADHI TU YA MADHARA YA POMBE KIAFYA. ACHA KUNYWA POMBE UIMARISHE AFYA YAKO.

 

mzunguko.com

 

By Mwanahamis Mkali.

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload