YANGA YAITUMIA SALAMU SIMBA OKTOBA 28.Ajibu awa tishio kubwa..

Klabu bingwa ya Ligi kuu Tanzania bara misimu mitatu mfululizo Young African(YANGA)Leo imeendelea kujichukulia alama muhimu katika ligi kuu ya Tanzania vodacom premier league baada ya kuirarua nyumbani timu ya Stand United ya mjini shinyanga.

Mchezo huo uliokuwa mtamu na kusisimua ulipigwa majira ya saa 10 kamili jion mjini huko,matokeo ya mchezo yamekuwa magumu kwa upande wa stand unuited baada ya kukubali kichapo kikali wakiwa nyumbani dhidi ya mabingwa watetezi hao.


Si mwingine bali alikuwa Mshambuliaji ya Yanga Ibrahimu ajibu migomba aliyeifanya yanga kutangualia kwa magoli maridadi 2 ya kipindi cha kwanza,huku mengine yakifungwa na Obrey Chirwa na Buswita hivyo mpaka kipenga cha mwisho magoli yakabaki hivyo huku Yanga wakiondoka na alama tatu muhimu.


Wiki ijayo tarehe 28 Yanga atakutana na mtani wake wa jadi Simba,timu ya Simba ambayo ndo vinara wa ligi hii mpaka sasa baada ya jana kuchukua alama tatu muhimu ndani ya uwanja wa uhuru.mchezo huo utakuwa mkali sana na wa kusismua sana kwan timu zote zinaonekana zimepaniana.NA:Sam Kameme

mzunguko.com

mzunguko.com


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu