EVERTON WAMFUKUZA KOCHA WAO....Timu ya soka ya nchini uingereza waliofanya ziara kabambe hapa nchini Tanzania Everton wamemfungisha virago kocha wao Ronald Koeman baada ya kupokea kichapo cha goli 5-2 kutoka kwa Arsenal wikiendi iliyopita,


Everton wamekuwa na mwanzo mbovu wa msimu wa ligi baada ya kutopata matokeo mazuri katika mechi za mwanzo wa msimu.Licha ya kuwa na mshambuaji wao hatari tokea Manchester United Wayne Roney bado safu ya ushambualiaji wa timu hiyo imeoneakana kuwa butu kiasi cha kushindwa kupata matokeo mazuri wawapo uwanjani.


Ronald Koeman aliyechukua virago vya Roberto Martinez bado hakuwa na msimu mzuri sana na timu hiyo kwani ana ushindi wa asilimia 40 tu tangua apewe timu hiyo.


Licha ya kusajili maingizo mapya bado ameshindwa kufanya vyema na timu hiyo inayoboronga baada ya kumuuza mshambuliaji wake hatari sana msimu uliopita Romeru Lukaku.mzunguko.com


Na:Sam kameme


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu