DK KIGWANGALLA AFUTA VIBALI VYA UWINDAJI,,,Waziri wa Maliasili na Utalii, Hamisi Kigwangalla amefuta vibali vyote vya uwindaji kwa kampuni kuanzia Octoba 22/2017 na kutoa siku 60 kwa watendaji ili waratibu mchakato upya utakaowezesha vitalu kugawiwa kwa mnada.

Mbali na hivo, Dk Kigwangalla pia amemwagiza katibu mkuu wa wizara hiyo, ndani ya muda mfupi kuwaandikia Hazina ili kuzichukua hoteli 10 kati ya 17 zilizobinafsishwa ambazo zimeshindwa kutimiza masharti.

Ametoa maagizo hayo jana alipohitimisha mazungumzo na wadau wa sekta ya utalii na maliasili aliokutana nao mjini Dodoma.

“ Kwa mamlaka niliyonayo katika sheria, natamka kwamba, nafuta rasmi vibali vyote vya uwindaji kwa Kampuni vilivyotolewa na wizara yangu kwa mwaka huu. Pia naagiza watendaji wote wanaosimamia hili wahakikishe wanaandaa mchakato ndani ya siku 60 illi mnada ufanyike na uwe wa uwazi.”, aliagiza Dk Kigwangalla.

Licha ya kuongelea kuhusu ufutaji wa vibali, alihamia upande wa vitalu vyeye migogoro vikiwemo vya Loliondo na Natron, ameagiza visigawiwe hadi migogoro itakapokwisha.


mzunguko.com

NA MWANAHAMIS MKALITufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu