Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

"VIJANA ACHENI KUCHAGUA KAZI"..Mh Mwita

October 23, 2017

 

 

 

Vijana jijini Dar es salaam wanapaswa kuacha tabia ya kuchagua kazi za kufanya, kwa lengo la kusubiri ajira kutoka serikalini jambo ambalo sio sawa, wanapaswa kufanya shughuli yeyote ambayo itawaingizia kipato na kuweza kuendesha maisha yao. Hasa kwa wanafunzi waliohitimu na kusubiri ajira kutoka srikalini.

 

Hayo yamezungumzwa na Mstahiki Meya wa jiji la Dar es salaam Isaya Mwita alipokuwa akitoa hotuba kwenye mahafali ya kidato cha nne shule ya sekondari  Minazini iliyopo Kata ya Vijiweni, Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni.

Aidha Meya Mwita amewaasa wanafunzi hao wanaohitimu kufanya kazi na kuacha kuchagua kazi kwani kazi ni kazi tu ilimradi inakuingizia kipato cha kuendesha maisha na iwe halali ambayo haivunji sheria.

 

mzunguko.com

 

By MWANAHAMIS MKALI.

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload