Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

TUNDU LISSU“WANA MBEYA NA WATANZANIA WOTE WAJIANDAE”

October 23, 2017

 

.

 

 

Mbunge wa Mbeya Mjini kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo( CHADEMA) Mh. Joseph Mbilinyi amesema kuwa ameagizwa na Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu kuwaambia wana Mbeya   na Watanzania kwa pamoja kuwa wjiandae.

Hayo yamezungumzwa baaada ya Joseph Mbilinyi kumtembelea Tundu Lissu jijini Nairobi nchini Kenya na kusema kutokana na uimara ambao Tundu Lissu anao amewataka Watanzania kujiandaa.

“’ Nimemtembelea ‘Big hommie’, Nairobi hospitali. Ameniambia nikawaambie wana Mbeya kuwa alisikia mwitikio wao wa kishindo nilipomtaja kwenye jukwaa la muziki na kuwa mwili wake ‘uliovunjwa vunjwa’ kwa risasi unazidi kuimarika na atasimama tena. Ameniagiza niwaambie wana Mbeya na Wanatanzania wote wajiandae, wajiandae, wajiandae” alisema Sugu.

Katika safari hiyo ya kumtembelea Tundu Lissu, Mh. Mbilinyi, alikuwa pamoja na Mbunge wa Iringa Mjini siku ya  Ijumaa jijini Nairobi Kenya anapopatiwa matibabu baada ya kushambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana  akiwa nyumbani kwake mjini Dodoma Septemba 7,2017.

 

mzunguko.com

 

By MWANAHAMIS MKALI

 

 

 

 

 

 

 

                                       

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload