Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

DK KIGWANGALLA AFUTA VIBALI VYA UWINDAJI,,,

October 23, 2017

 

 

 

 

 

 

 

Waziri wa Maliasili na Utalii, Hamisi Kigwangalla amefuta vibali vyote vya  uwindaji  kwa kampuni kuanzia Octoba 22/2017 na kutoa siku 60 kwa watendaji ili waratibu mchakato upya utakaowezesha vitalu kugawiwa kwa mnada.

Mbali na hivo, Dk Kigwangalla pia amemwagiza katibu mkuu wa wizara hiyo, ndani ya muda mfupi kuwaandikia Hazina ili kuzichukua hoteli 10 kati ya 17 zilizobinafsishwa ambazo zimeshindwa kutimiza masharti.

Ametoa maagizo hayo jana alipohitimisha mazungumzo na wadau wa sekta ya utalii na maliasili aliokutana nao mjini Dodoma.

“ Kwa mamlaka niliyonayo katika sheria, natamka kwamba, nafuta rasmi vibali vyote vya uwindaji kwa Kampuni vilivyotolewa na wizara yangu  kwa mwaka huu. Pia naagiza watendaji wote wanaosimamia hili wahakikishe wanaandaa  mchakato ndani ya siku 60 illi mnada ufanyike na uwe wa  uwazi.”, aliagiza Dk Kigwangalla.

Licha ya kuongelea kuhusu  ufutaji wa vibali, alihamia  upande wa vitalu vyeye migogoro vikiwemo vya Loliondo na Natron, ameagiza visigawiwe hadi migogoro itakapokwisha.

 

mzunguko.com

 

 

 

NA MWANAHAMIS MKALI

                                                                       

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload