TOTENHAM YAICHABANGA LIVERPOOL KIPIGO CHA MBWA MWIZI.......Baada ya kuoa sare ya 1-1 na Real Madrid wa Uhispania timu ya soka ya ligi kuu Uingereza Totenham imeicharaza vikali timu toka mji wa liverpool kwa mabao 4-1,

Mechi ya leo ilitegemea kutoa upinzani mkali sana kwani timu hizo zimeonekana bora hasa katika upande wa ligi mabingwa ulaya ambapo mechi hizo zimechezwa katikati ya wiki bila kupoteza kwa timu hizo.


Magoli ya Harry Kane dakika ya 4,56,Son dakika ya 12,na msumari wa nne ulitiwa kimiani na Delle alli dakika ya nyongeza baada ya kipindi cha kwanza (48),goli la majogoo liver lilifungwa na mshambuaji hatari M sallah dakika ya 24 .

Matokeo hayo yanaifanya liverpool kushika nafasi ya 09 katika msimamo wa ligi kuu nchini humo wakiwa na pointi 13.


mzunguko.comTufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu