OKWI AZIDI KUPAA KILELENI SIMBA IKIFANYA MAUAJI......AZAM YAKABWA KOO NA MBAO,MBEYA CITY,MTIBWA ZAPE

Emanuel Okwi amefunga goli la nane katika mechi yake ya sita ya ligi kuu Tanzania bara msimu huu wakati Simba ikishinda 4-0 dhidi ya Njombe Mji.

Okwi ameendeleza utawala kwenye uwanja wa Uhuru, magoli yake yote (8) ameyafunga kwenye uwanja huo. Mchezaji pekee mwenye magoli mengi aliyofunga kwenye uwanja mmoja.

Amefunga mechi nne mfululizo ambazo Simba imecheza kwenye uwanja wa Uhuru, hajafunga katika mechi mbili ambazo amecheza nje ya uwanja wa Uhuru.

Simba 7-0 Ruvu Shooting (Okwi alifunga magoli manne, akawa mchezaji wa kwanza kufunga hat-trick msimu huu.)

Simba 3-0 Mwadui (alifunga magoli mawili na kufikisha magoli sita)

Simba 1-1 Mtibwa Sugar (akaendeleza rekodi ya kufunga mfululizo kwenye uwanja wa Uhuru na kufikisha magoli saba yote akiyafunga uwanja huohuo.)

Simba 4-0 Njombe Mji (Okwi alifunga goli (1) la kwanza katika mchezo huo.

Raia huyo wa Uganda aliifungia Simba bao la kwanza kwa kichwa kipindi cha kwanza huku Mzamiru Yassin akipinga mbili naLaudit Mavugo akimaliza goli la nne.

Simba imefikisha pointi 15 sawa Mtibwa Sugar ambao wameshinda 1-0 dhidi ya Tanzania Prisons lakini ‘mnyama’ anaongoza ligi kwa tofauti ya magoli.

Matokeo ya mechi nyingine zilizochezwa leo

  • Mtibwa Sugar 1-0 Tanzania Prisons

  • Ndanda 0-0 Singida United

  • Mbao 0-0 Azam

  • Lipuli 1-0 Majimaji

  • Mbeya City 2-0 Ruvu Shooting

CHANZO:SHAFFI


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu