BOMU LAUA ZAIDI YA WATU 50 AFGHNISTAN

October 21, 2017

Takriban watu 39 wamekufa kufuatia shambulizi la bomu la kujitoa muhanga katika msikiti wa waumini wa Kishia katika mji mkuu wa Afghanistan Kabul. Shambulizi hilo lilifanyika ndani ya jengo lililopo mashariki mwa mji huo wakati waumini wakiwa katika kusanyiko la ibada ya jioni. Duru za kiusalama zinasema idadi ya vifo inaweza kuongezeka mara mbili kutokana na ukali wa mlipuko wa bomu hilo. Mapema jana ijumaa bomu jingine lililotegwa katika msikiti unaotumiwa na waumini wa madhehebu ya Sunni uliopo jimbo la kati la Ghor pia lilisababisha mauaji ya zaidi ya watu 30. Rais wa Afghanistan Ashraf Ghani ametoa hotuba ya kulaani mashambulizi hayo akisema kwamba vikosi vya usalama vya taifa hilo wataingilia kati mashambulizi hayo ili kuwaondosha magaidi wanaowalenga Waafghanistan wa dini na kabila zote.

 

mzunguko.com

 

CHANZO:DW

 

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon