TUNDU LISU AONEKANA KWA MARA YA KWANZA.

Hatimaye Tundu Lissu ametoa kauli ya kwanza iliyorekodiwa na kuambatanishwa na picha zinazomuonyesha akiwa amekaa na mwenye tabasamu, huku sauti ikiwa imara.


ikumbukwe kuwa ni takribani mwezi mmoja na siku kadhaa tangu mbunge wa Singida Mashariki Muheshimiwa Tundu Lissu aliposhambuliwa nyumbani kwake Dodoma akiwa anatokea katioka shughuli zake za kibunge jijini hapo na kupelekea majeraha makubwa katika mwili wake.


Jana jioni kwa mara ya kwanza imeonekana video picha ya muheshimiwa Lissu na sauti yake ikiwashukuru watu mbalimbali waliomuombea na kumsaidia kwa njia moja hata nyingine ili kuokoa maisha yake kwa kipindi chote alichokuwa mahututi.


Katika video hiyo ya sauti muheshimwa Lissu amesema ni Mungu tu ndo ameyaokoa maisha yake siku ile aliposhambuliwa na watu wasiojulikana akitaka kushuka toka kwenye gari nyumbani kwake Dodoma kwani Mungu alisema ,HATOKUFA BALI ATAISHI"hivyo ni mungu tu ndo kamponya.


Katika video sauti hiyo iliyoambatana na vipande mbalimbali vya picha muheshimiwa Lissu amewashukuru watu wote wakiwemo madaktari wa hospitali ya dodoma,hospitali ya Nairobi pamoja na viongozi mbalimbali walioenda kumsalimia akiwa hoi kitandani.


Mbali na Ubunge muheshimiwa lisu ni Mwanashria mkuu wa Chama cha demokrasia na maendeleo pia ni Raisi wa chama cha wanasheria Tanzania(TLS).

Muheshimiwa Lissu alimiminiwa risasi zipatazo 30 huku risasi tu zikiingia ndani ya mwili wake akitokea katika shughuli zake za kibunge mjini Dodoma.


Watanzania wote tunamtakia afya njema na Mungu ampe nguvu arudi katika majukumu yake ya kila siku ya kuwatumikia wananchi na Taifa kwa ujumla.


Na.Sam Kameme.


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu