CHAMA CHA USHIRIKA MFAVESCO KIMELETA MUONEKANO MPYA SOKO LA MWANANYAMALASoko la mwananyamala almaarufu kama MAPINDUZI Mkoani Dar Es Salaam, limeanzisha chama cha ushirika kiitwacho MFAVESCO LTD{ Mwananyamala Food and Vegetable Suplies Cooparative Society Limited), kwa lengo la kuboresha soko hilo.


Licha ya kuundwa kwa chama hicho, bado hawajapata mfadhili wa kuwasimamia na kuwasaidia katika uboreshwaji wa soko hilo. Msaada pekee ni uchangishwaji wa pesa kwa wafanya biashara wa soko pamoja na Bodi ya viongozi wa hapo.

Mwenyekiti wa soko hilo Mh. Juma Yusuph Musa amesema kuwa soko hilo limejaa bidhaa za nafaka kuliko bidhaa za aina nyingine kulingana na mahitaji ya wateja wao.

Hata hivyo mwenyekiti huyo ameongeza kuwa wanapata changamoto katika usafirishaji wa nafaka kutoka mikoani. Hususani katika bei za bidhaa na njia za uchukuzi {barabara}.


“ Soko letu limejaa bidhaa za nafaka kulingana na mahitaji ya wateja, Nafaka hizo zinatoka mikoani . Changamoto moja wapo ni usafirishaji wa mizigo. kutoa lori mkoani hadi huku ni gharama kubwa, na likishavuka Tan Roads na kuingia Barabara ya Manispaa ni lazima garii ikate kibali cha kupita Barabara hiyo” Amesema Mwenyekiti

“ Tukiangalia gharama za usafirishaji kutoka mikoani mpaka sokoni, na bei wanazohitaji wanunuzi wa bidhaa kwa kweli faida ni kidogo. Tunaomba Serikali ituangalie katika hilo” Aliongeza Mwenyekiti.


By Mwanahamis ,Mkali

mzunguko.com


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu