Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

CHAMA CHA USHIRIKA MFAVESCO KIMELETA MUONEKANO MPYA SOKO LA MWANANYAMALA

October 19, 2017

 

 

 

 

 

Soko la mwananyamala almaarufu kama  MAPINDUZI Mkoani Dar Es Salaam, limeanzisha chama cha ushirika kiitwacho MFAVESCO LTD{ Mwananyamala Food and Vegetable Suplies Cooparative Society Limited), kwa lengo la kuboresha soko hilo.

 

Licha ya kuundwa kwa  chama hicho, bado hawajapata mfadhili wa kuwasimamia na kuwasaidia katika uboreshwaji wa soko hilo. Msaada pekee ni uchangishwaji wa pesa kwa wafanya biashara wa soko  pamoja na Bodi ya viongozi wa hapo.

Mwenyekiti wa soko hilo Mh. Juma Yusuph Musa amesema kuwa soko hilo limejaa bidhaa za nafaka  kuliko bidhaa za aina nyingine kulingana na mahitaji ya wateja wao.

Hata hivyo mwenyekiti huyo ameongeza kuwa wanapata changamoto katika usafirishaji wa nafaka kutoka mikoani.  Hususani katika bei za bidhaa na njia za uchukuzi {barabara}.

 

“ Soko letu limejaa bidhaa za nafaka kulingana na mahitaji ya wateja, Nafaka hizo zinatoka mikoani . Changamoto moja wapo ni usafirishaji wa mizigo.  kutoa lori  mkoani hadi huku ni gharama kubwa, na likishavuka Tan Roads na kuingia Barabara ya Manispaa ni lazima garii ikate kibali  cha kupita Barabara  hiyo” Amesema Mwenyekiti

“  Tukiangalia gharama za usafirishaji kutoka mikoani mpaka sokoni, na bei wanazohitaji wanunuzi wa bidhaa   kwa kweli faida ni kidogo. Tunaomba Serikali ituangalie katika hilo” Aliongeza Mwenyekiti.

 

By Mwanahamis  ,Mkali

 

mzunguko.com

 

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload