TAKUKURU WAMPA NASSARI ONYO KALI.Taasisi ya Kupambana na kuzuia Rushwa nchini Tanzania(TAKUKURU)Imemuagiza mbunge wa Arumeru Mashariki kutulia kupisha uchunguzi wa tuhuma zilizowakilishwa na mbunge huyo machachari wa Chadema dhidi ya kupewa rushwa kwa madiwani wa chama hicho waliohamia Chama Cha Mapinduzi.


Hayo yamesemwa na Mkurugenzi mkuu wa TAKUKURU Valentino Mlowola alipoongea na waandishi wa habari ofisini kwake jana.Aidha Mkurugenzi huyo amemuonya mbunge huyo kutowashinikiza kwani. kufanya hivyo ni kinume na sheria na akiendelea hivyo watamchukulia hatua za kisheria bila kuathiri taarifa alizozipeleka kwenye taasisi hiyo.


Mlowola amesema kwamba Taasisi ya kupambana na rushrwa (TAKUKURU) inayafanyia taarifa ya kupewa rushwa kwa madiwani waliotangaza kuhamia chama tawala ulioletwa na Mh Nassari ofisini kwao hivyo atulie apishe uchunguzi ufanyike ili hatua zaid zichukuliwe kwani anachokiwasilisha Nassari sio ushahidi ni taarifa.


Aliongeza kwa kusema swala hilo sio la kisiasa hivyo Mbunge huyo aache kulipeleka kisiasa kwani taasisi yao ni huru na haiingiliwi na chombo chochote kwa mujibu wa sheria ,Pia mkurugenzi ameshangazwa na mtindo anaoutumia Mh Nassari wa kuwasilisha taarifa zake za rushwa katika vyombo vya habari badala ya kuwasilisha sehemu husika.


Ikumbukwe kuwa muheshimiwa Nssari alifika katika ofisi za TAKUKURU oktoba 2 kuwasilisha alichodai kuwa ni ushahidi wa kuhongwa kwa madiwani wa Chadema kuhamia Chama cha Mapinduzi (CCM)


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu