Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

WAKAZI WA CHAMAZI WAMPIGIA MAGOTI PAUL MAKONDA

October 18, 2017

 

 

Wakazi  wa mji mpya wa Chamazi uliopo Mbagala nje kidogo ya jiji, wamemuomba mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda kufanya ziara ya kustukiza ili ajionee uzembe wa watendaji wa serikali.

   

  Kwa nyakati tofauti wakazi wa eneo hilo wameyataja matatizo yao kwamba ni kuachwa kushughulikiwa kwa barabara za mitaa ambazo baadaye zimegeuka mabonde makubwa  yaliyopeleka maji katika mabonde yaliyokuwa  yakichimbwa mchanga.

     

“Mbaya zaidi barabara hizo zimewekewa nguzo kubwa za umeme ambazo zipo hatarini kuanguka katika kipindi cha mvua” Alisema mjumbe wa mtaa wa Dovya, Suleimani Bakari.

 

Na Mwanahamis Mkali

 

    

   

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload