Tufuate kupitia:
 • YouTube Social Icon
 • Twitter Social Icon
 • Black Instagram Icon
 • Facebook Social Icon

MADRID VS TOTENHAM HAKUNA MBABE,LIVER,MAN CITY WAPETA USIKU WA ULAYA.

October 18, 2017

 

 

 

 

Jana usiku ligi ya mabingwa ulaya  ilitimua vumbi huku timu mbaliombali zikishuka dimbani kuonyeshana ubabe wa vikosi vyao,miamba hiyo ya soka ya ulaya ilikutana katika michezo iliyopigwa nyumbani na ugenini,

 

Mabingwa wa Hispania na ligi ya mabingwa msimu uliopita  Real Madrid wakiongozwa na kocha wao Zinedine Zidane(zizzou) walishindwa  kuonyesha ubabe mbele ya timu bishi toka ligi kuu  Uingereza Totenham Hotspur kwa kutoshana nguvu, hadi mwisho wa mchezo matokeo yakabaki 1-1.Magoli ya yote yalipatikana kutoka kwa wachezaji wa Real Madrid.Beki kisiki Raphael Varane alijifunga  dakika ya 28 baada ya mpira uliopigwa na mawinga wa Totenham   kumbabatiza  na kumwacha kipa wa miamba hiyo ya Hispania asijue la kufanya,Goli  la kusawazishala Real Madrid lilifungwa na mshambuliaji hatari wa Real Madrid Christiano Ronaldo dakika 43 ya mchezo kwa njia ya mkwaju wa penalti na hivyo kufanya matokeo ya sare mpaka kipenga cha mwisho wa mchezo.

 

Michezo mingine iliyopigwa ilikuwa kati ya Man City na Napoli,na miamba ya soka ya Uingereza Kuibuka na ushindi mnono wa 2-1,magoli ya Man city yaliwekwa kimiani na Rahim sterling 09,na Gabriel Jesus 13.

Pia jana ilikuwa ni siku muhimu kwa Majogoo wa London baada ya kumtandika Maribor goli 7-0 huku wachezaji wa liver wakionyesha uwezo mkubwa zaidi katika mchezo huo.Magoli ya Firmino (4,54), M Salah (19,39)Coutinho(13),Chamberlain(86),Alexander arnold (90).

 

Leo kutakua na michezo mingine ya UEFA CHAMPION LIGUE  huku timu mbalimbali zikitafuta uongozi wa makundi yao ili kusonga mbele,

 

 • CL Qarabag 17:00 A Madrid

 • CL Anderlecht 19:45 PSG

 • CL Barcelona 19:45 Olympiakos

 • CL Bay Munich 19:45 Celtic

 • CL Benfica 19:45 Man Utd

 • CL CSKA Mosc 19:45 Basel

 • CL Chelsea 19:45 Roma

 • CL Juventus 19:45 Sporting

Imeandaliwa na :Sam Kameme.

mzunguko.com.

 

mz

I

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload