KWAHERI KAKA' UMEUTENDEA MPIRA HAKI, PUMZIKA SASA.

October 18, 2017

 

 

 

 

 

 

 

Ricardo Izecson Dos Santos Leite(KAKA’)

 

Alianza kuwa maarufu baada ya kombe la Dunia la mwaka 2002 nchini japan na Korean kusini akiwa na umri wa miaka 20,na jina lake kuanza kuingia katika msikio ya wapenda soka  duniani kote na ulimwengu mzima kuanza kumfahamu kijana huyu aliyebariki kipaji toka  Nchi ya soka  Brazili,Miaka ya 2006/2007 alikuwa mchezaji  ambaye kila mtu aliamini kwamba mipira ilikuwa ikiisikiliza miguu yake, ilisemekana alikuwa na uwezo wa kuambia mpira toka hapa nenda pale na mpira ukatii.

 

Wapenda soka wengi duniani kote waliamini hivyo kutokana na uwezo wake mkubwa aliokuwa akiounesha uwanjani na sio siri alimfanya kila kijana atamani kucheza mpira kwani aliufanya mpira uonekana kazi rahisi sana ukiwa unatumia akili.

 

KAKA’ ni  mzaliwa wa Gama mwaka 1982 mchezaji ambaye wazi wazi ilionekana kwamba mungu alikuwa na mpango juu ya miguu yake na ndio maana pamoja na majeraha makubwa akiwa mtoto lakini bado alipiga soka.

 

 

Jina la Kaka lilianza  kuvuma sana wakati akiwa bado yuko Sao Paulo lakini umaarufu uliongezeka zaidi mwaka 2003 wakati anajiunga na Ac Millan kuchukua nafasi ya Rui Costa kwa ada ya £8.5m na hapo dunia nzima ikaanza kushangaa uwezo wa Mbrazil huyu.

 

Akicheza pamoja na Andriy Shevchenko, Pipo Inzaghi na John Dahl Thomason aliifanya Rossoneri waonekane kama klabu ambayo haikuwa na namna ya kuzilika kukufunga kwani uwepo wake nyuma ya mtu kama Shevchenko ilikuwa ndoto ya kutisha kwa wapinzani.

 

Mwaka 2007 Kaka alichukua tuzo ya mchezaji bora wa dunia  mbele ya Christiano Ronaldo na Lionel Messi  na  kuipeleka nyumbani kwao Sao Paulo ambako watu walimshukuru mungu kwa tuzo hiyo.

 

Inaaminika kuwa kaka hajawahi kushiriki tendo la ndoa hadi mwaka 2008 ambapo ndio mwaka aliomuoa mke wake na mpenzi wa muda mrefu Carolline Celico na kuanzisha familia na binti huyo mrembo sana na kubarikiwa na mungu watoto.

 

 

Safari ya Real Madrid ndio ulikuwa mwanzo wa Ricardo Kaka kupotea mchezoni kwani tangu ajiunge nao majeruhi yamekuwa yakimuandama kila siku huku akizungukwa na washambuliaji wengi wakubwa Rafael Van De Vaart, Karim Benzema, Raul Gonzalez, Gutti na Gonzalo Higuain.

 

 Kaka hakuwa na tamaa ya pesa wala tamaa za kimwili ila alikuwa mtu wa kupenda ibada tofauti na wachezaji wengi wa kibrazili ambao mara nyingi hutajwa katika kashfa za wanawake na anasa kupitiliza.Kaka alikuwa akitoka mazoezini hurudi nyumbani kwake na kusikiliza nyimbo za dini.

 

Majeraha yalipopitiliza ndani ya Bernabeu huku Madrid wakimuongeza nyota mpya Cr7 kikosini vilimfanya Kaka mwaka 2013 kurejea Millan na kisha akarudi nyumbani kwao Sao Paulo kwa mkopo kucheza kwa muda kabla ya kwenda Orlando City alikomalizia soka lake.

 

Carlos Alberto Perreira alikuwa kocha wa kwanza kumuita Kaka katika timu ya taifa na pamoja na majeraha ya mara kwa mara lakini alifanikiwa kuichezea timu ya taifa michezo 92 idadi sawa na Pele na kubwa kuliko Rivaldo, Neymar, Dida na Dunga.

 

Kaka hupendelea zaidi kusoma Biblia kuliko kitabu kingine chochote,na huyo ndo mtumishi wa mungu na mchezaji mpira wa miguu nguli kutoka Brazili aliyekipiga katika timu bora zaidi duniani kma AC Milan,Real Madrid na Orlando city.

 

mzunguko.com

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon