Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

JOTO LA UCHAGUZI KENYA LAZIDI KUWA JUU,KAMISHNA UCHAGUZI AJIUZULU NAFASI YAKE.

October 18, 2017

 

Zikiwa imebaki wiki moja na siku kadhaa  Kenya kuingia kwenye uchaguzi mkuu wa marudio baada ya ule wa awali kufutwa mambo yameendelea kuwa sio mazuri sana kwa upande wa Tume ya Uchaguzi ya nchini Kenya(IEBC) Baada ya Kamishna wa uchaguzi kujiuzulu nafasi yake hiyo.

 

Dr Roselyn Akombe ametuma Waraka huo wa kujiuzulu akiwa nchini Marekani anapoishi, Dr akombe aliyekuwa mfanyakazi wa umoja wa mataifa kabla ya kuteuliwa kuwa kamishna wa Tume hiyo ya uchaguzi ya nchini Kenya.

Dr Akombe amedai kwamba  Uchaguzi wa marudio unaopangwa kufanywa wiki mbili zijazo bado haujakidhi vigezo vya kuwa huru na wa haki.

 

Dr Roselyn Akombe Kwamboka ni mzaliwa wa Kenya 1976 katika akaunti ya Nyamira na kusomea katika chuo kikuu cha Nairobi na badae kuelekea Marekani kwa ajili ya masomo zaidi.

 

Ametumikia umoja wa mataifa kama katibu nafasi ambayo imempa uzoefu mpka kuchaguliwa kwake kama kamishna wa uchaguzi mkuu wa Kenya ambao ulifanywa miezi kadhaa iliyopita kbala ya kufutwa na kutangazwa kurudiwa na jopo la majaji kwa kubainika kuwa na kasoro kadhaa.

 

mzunguko.com

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload