WAHITIMU VYUO VIKUU WANUFAIKA NA MKAKATI WA DANGOTE.


Mfanyabiashara mkubwa ,maarufu barani Africa na Tajiri namba moja wa bara la Africa Bwana Aliko Dangote(Dangote) amedhamiria kufanya kitu cha tofauti katika bara hili na nchi yake kwa ujumla baada ya kuweka bayana mpango wake wa kuanzisha kilimo cha mpunga na usambazaji. Mpango huo unaotekelezwa na kampuni yake ya Dangote Rice Limited iliyojikita kwenye kilimo hicho,katika Jiji la Kogi nchini Nigeria, unalenga kupunguza uhaba wa ajira kwa wahitimu hao na kupambana na baa la njaa katika bara la Africa na nchi ya Nigeria.


Katika utekelezaji huo kampuni hiyo itawashirikisha wahitimu wa vyuo vikuu ili kulima hekta 100 kwa ahadi ya kununua mpunga utakaozalishwa huku yenyewe ikitoa mbegu, ushauri wa namna ya kukabiliana na changamoto za kilimo, viuatilifu na mbolea.


Akiwakilisha mkakati huo Mkurugenzi Mtendaji wa Dangote Rice, Devakumar Edwin alisema mradi huo ni sehemu ya kuwaandaa wajasiriamali watakaoleta mapinduzi kwenye sekta ya kilimo na kuongeza uzalishaji wa sekta hiyo kwa kiwango kikubwa.


Mkurugenzi huyo alisema, “Tunaamini ujuzi, maarifa, mazingira rafiki na ushirikiano katika mnyororo wa thamani ni miongoni mwa mambo yatakayofanikisha mapinduzi ya kilimo. Mradi huu utatatua changamoto ya maarifa yanayohitajika katika uzalishaji wa mpunga miongoni mwa vijana,”

Mkurugenzi huyo aliwataka vijana hao kujikita kwenye kilimo hicho ili kukuza kipato na ustawi wa familia zao. Mradi una zaidi ya hekta 25,000 za wakulima wadogo na mpaka mwakani, unatarajiwa kuanza kuzalisha tani milioni moja za ujazo.Wasomi na watu mbalimbali wamepongeza hatua hiyo ya mfanyabiashara huyo kwa kuwakumbuka wasomi ambao watanufaika na mradi huo kwa kiasi kikubwa katika kipindi hichi ambacho ajira ni tatizo kubwa katika nchi nyingi za kiafrika.Ikumbukwe Nigeria ni moja ya nchi yenye tatizo kubwa la uhaba wa ajira kwa vijana wake wengi wao wakiwa ni wasomi na wahitimu vyuo vikuu.

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu