Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

MFAHAMU ALIYEWAUA AC MILAN KWENYE DERBY DELLA MADONNINA.

October 17, 2017

 

 

 

Jina lake kamili ni “Mauro Emanuel Icardi Riveiro”hakika kwa wikiendi  iliyopita ilikuwa na uchungu sana kwa mashabiki wa timu ya mpira ya AC Milan ya nchini Italia,hii ni baada ya mahasimu wao  kukutana  katika ligi kuu ya nchini humo.Mahasimu hao wa jijini Milan kwa pamoja hutumia uwanja wao wa nyumbani ujulikanao kama SAN SIRRO kwa AC MILAN au STADIO GUISEPE  MEAZZA kwa Inter Milan jina ambalo wameupa Inter Milan uwanja huo kumuenzi  mchezaji wao gwiji wa  zamani, Mchezo huo namba 290 ulipigwa mnamo majira ya saa 3:45 usiku

 

Mchezo wa inter Milan na AC Milan hujulikana zaidi kama Derby Della Maddonina kama nilivyoandika hapo awali ,Mauro Emanuel Ircard Riveiro ndo jina alilopewa kijana huyo mwenye kipaji cha pekee pale inter,mwenye uraia wa nchini Argentina miaka 24 iliyopita,Ana urefu wa futi 5 na inchi 11,anavaa jezi nmba 9 ya wakali hao wa jiji la Milan na kwa sasa ndiye kapteni wa miamba hiyo ya soka ya nchini italia baada ya juventus kuwasumbua kwa muda mrefu.

 

Alianza soka lake katika klabu ya Vecindario (2002-2008),Barcelona (2008-2011),Sampdoria (2011-2012),Inter Milan 2013-Katika mchezo wa juzi Mchezaji huyu aliibuka shujaa baada ya kuifungia timu yake magoli matatu(hat trick) wakati timu yake ilipoibuka na ushindi wa 3-2 dhidi ya mahasimu wao toka jiji moja la jijini hapo Milan.goli la dakika za mtoto halali na pesa bali nepi likaipa pointi tatu muhimu timu ya inter milan.

 

Icardi alizaliwa jijini Rosario Argentina kabla ya kutimkia Nchini Hispania akiwa na umri wa miaka 9 na alijiunga na timu ya watoto Vecindario na alifunga jumla ya mgoli 500 katika utoto wake wa kucheza soka,

 

Mwaka 2007 miamba ya soka ya barcelona iliinyaka saini ya kinda huyo baada ya kutakiwa na timu nyingi ikiwemo Real madrid,valencia,seviil,espanyol  Arsenal na liverpool,Hakufanya vizuri sana akiwa katika timu hiyo ya Barcelona baada ya kukosa nafasi katika kikosi cha wakubwa  kutokana na kikosi hicho kujaa nyota na kushindwa kushindana nao.hivyo alicheza na makinda wa barcelona

 

Baada ya kushindwa kuingia katika timu ta wakubwa ya vijana toka catalan Ircardi alitimkia Sampdoria kwa mkopo toka mwa 2011 na kufunga magoli 13 katika mechi 19,alifunga goli  lake la kwanza kama mchezaji wa kulipwa pmnamo may 12 mwaka 2012 kwenye ushindi wa 2-1 kwa timu yake. 

 

 

 

Mwanzo mwa msimu wa 2014 alitangazwa kama mchezaji wa inter Milan kwa ada ya uhamisho wa Euro milion 6 kwa kukamilika kwa haki zote kwa asilimia 50. Alipata majeruhi na kukaa nje ya uwanja  mpaka mnao mwaka 2014 kabla ya kurudi uwanjani na kufunga goli dhidi ya  fiorentina ikiwa mechi yake y kwanza  baada ya majeruhi.

 

Alitangazwa kapteni wa inter milan mwaka 2015 akichukua nafasi ya Andrea Ronnochia,mwaka Icardi amesaini mkataba na inter milan mpaka mwaka 2021 huku akivuna mshahara wenye thamani ya Euro milion4.5 kwa mwaka.huku ndoto zake ni kutwaa mataji na timu hiyo nguli ya Italia.

 

Huyo ndo Mauro Icardi aliyewanyima usingizi mashabiki wa AC Milan kwenye mchezo namba 290

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload