LEICESTER CITY WAMPIGA CHINI KOCHA WAO.

October 17, 2017

 

 

Klabu ya soka ya Leicester city ya nchini Uingereza imetangaza kuachan na kocha wake aliyedumu kwa miezi minne tu na timu hiyo,hiyo ni baada ya mwendelezo wa matokeo mabaya ya timu hiyo iliyotwaa ubingwa wa Ligi kuu nchini humo 2015/2016 chini ya kocha wake wa kipindi hicho Muitaliano Claudio Ranieri,

 

Craig Shakespeare (53,)aliiongoza klabu hiyo ya katika mchezo wao wa mwisho wa ligi kuu nchini humo juzi waliposuluhu kwa matokeo ya 1-1 dhidi ya West Brom ya nchini humo.

 

Baada ya matokeo mabovu kocha huyo aliitwa na uongozi wa timu hiyo siku ya jumanne na kujadili mwenendo wa timu hiyo na kuamua kumbwagisha manyanga kocha huyo baada ya mechi nane tu za ligi kuu ya nchini humo.

 

Makamu wa raisi wa klabu hiyo alithibitisha hilo na alisema"Craig amekuwa msaada mkubwa sana kwa timu tangu alipokuwa akihudumu kama kocha msaidizi na hata alipokabithiwa timu kama kocha mkuu  na kuitumikia klabu kwa mafanikio makubwa"pia akasema Craig atakumbukwa kama shujaa na mtu wa  heshima na anaheshimiwa na klabu,pia muda wowote anakaribishwa kwa ajili ya kazi au kwa ushauri kama rafiki  wa klabu hiyo.

 

Nafasi ya kocha huyo itachukuliwa na msaidizi wake Michae Aplleton kwa michezo itakayofata mpaka atakapotambulishwa kocha mpya

 

Chanzo;Independent News

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon