Wafalme wa Ulaya: Real Madrid C.F

June 5, 2017

 

 

Chini ya kocha Zinedine Zidane "Zizzou", tarehe 4 Juni timu ya Real Madrid kutoka Spain

ilifanikiwa kutwaa ubingwa wa kombe la Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kuifunga timu ya

Juventus kwa mabao  manne kwa moja (4 - 0).

 

Bao la kwanza lilifungwa na Christian Ronaldo katika dakika ya 20 baada ya kucheza moja mbili yaani nakupa nirudishie na Carvajal na kisha kupiga shuti kali bila kutuliza na kumuacha kipa mkongwe Gianluigi Buffon akitapatapa. Dakika saba baadae katika dakika ya 27, Mario Madzukic aliisawazishia Juventus kwa goli zuri sana la tikitaka. Goli ambalo watangazaji wa mechi walinena kama linastahili kwenda kushindanishwa kuwa goli bora la michuano na msimu.

 

 

 

Kipindi cha pili kilivyoanza mambo yakaanza kwenda kombo kwa Juventus wakiwa wanaonekana hawashambulii kama walivyofanya kipindi cha kwanza. Real Madrid kwa uzoefu wake akawa muda mwingi yupo golini kwa Juventus na hatimaye mnamo dakika ya 61, Casemiro aliiandikia Madrid bao la pili kwa shuti kali alilopiga akiwa nje ya boksi ya 18. Dakika nne baadae Christiano Ronaldo alifunga bao la tatu na kumkatisha tamaa kabisa kibibi kutoka Torino. Mnamo dakika ya 90, mchezaji kinda wa Real Madrid Marco Asensio aliengia kama mbadala wa Karim Benzema.

 

Christiano Ronaldo anaendeleza rekodi nzuri aliekuwa nayo. Hili ni kikombe chake cha nne cha Ubingwa Ligi ya Mabingwa Ulaya. 

 

 

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon