Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Volkswagen Kuanza Kutengeneza Magari Kenya

April 19, 2017

Baada ya miongo minne, mtengeneza magari maarufu duniani Volkswagen anaanza tena kutengeneza magari Kenya. Vw anatarajia kufungua kiwanda cha kutengeza magari kabla ya mwaka 2016 kuisha. Volkswagen anafanya hivi kama hatua ya kuuza magari mengi Zaidi Afrika Mashariki.

 

Volkswagen ni mzoefu katika masoko chipukizi kwani kashawahi kutumia mbinu hii nchini Mexico na gari alilotengeza modeli ya beetle lilipendwa sana na kuuzika sana nchini humo. Nchini Kenya Volkswagen ataanza na modeli ya Vivo na baadae kuendelea na modeli zinginezo.

 

“We believe that Kenya has got the potential to develop a very big fully-fledged automotive industry. The East African Community has got the potential, and today is the first step in this direction that we want to take with our passenger cars”, said Thomas Schafer, CEO Volkswagen South Africa.

 

“Tunaamini kwamba Kenya ina uwezo wa kutengeneza sekta ya kujitosheleza ya magari. Jamii ya Afrika Mashariki ina uwezo, na leo ndio hatua ya kwanza ya mwelekeo ambao tunaka twende na magari yetu ya abiria,” alisema Thomas Schafer, Afisa Mtendaji Mkuu, Volkswagen South Africa.

 

Bw Schafer pia akaongeza kuwa Kenya ina nafasi kuwa nchi inayouzia magari nchi nyingine za Afrika Mashariki.

 

Mtengeneza magari, Volkswagen aliwahi kufanya kazi Kenya  kuanzia 1960 mpaka 1977 na alikuwa anatengeza Volkswagen vans, mabasi madogo na gari maarufu Kombi.

Rais Kenyatta alisema kurudi kwa Volkswagen ni ishara ya mabadiliko ya kiuchumi ambayo Kenya inayapitia. Alisema jitihada hizi zitaleta kazi kwa wakenya wengi.

 

 Pichani Juu: Rais Kenyatta akiwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa VW South Africa

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload