Umuhimu wa Umoja wa Ulaya kutumia fedha ya aina moja.

February 13, 2017

 

 

 Euro ilitengenezwa kwasababu utumiaji wa fedha au sarafu ya aina moja unaleta faidi nyingi zaidi kuliko mfumo uliokuwepo mwanzoni ambapo kila nchi ndani ya Umoja wa Ulaya ulikuwa unatumia sarafu yake.  

Kwa kutumia sarafu moja, uwezekano wa thamani ya sarafu kupanda na kushuka kiholela unapungua na hata gharama ya kufanya biashara baina ya nchi inapungua hivyo soko linakua kubwa zaidi na lenye nguvu zaidi. Na pia hii inamaanisha ushirikiano zaidi baina ya wajumbe wa umoja huo hivyo uchumi kukua na kufaidisha nchi zote katika umoja huo. Wakati Umoja wa Ulaya unaanzishwa mnamo mwaka 1957, Nchi wajumbe katika umoja huo walikuwa wanatumia nguvu nyingi katika kujenga soko la pamoja (common market) kwaajili ya kuongeza biashara. Lakini, muda ulivyozidi kwenda, ikawa wazi kuwa ushirikiano wa mfumo wa fedha na uchumi ulikuwa unahitajika ili soko la pamoja lifanikiwe na liwe la maana zaidi ili kufanikisha uchumi wa Ulaya kuwa na nguvu zaidi na kutengeneza kazi nyingi zaidi kwa bara nzima la Ulaya. Mnamo mwaka 1991, wajumbe wa umoja huo walipitisha makubaliano ya Maastrucht ambapo makubaliano hayo yaliamua kuwa Nchi wajumbe wa Umoja wa Ulaya watakuwa na sarafu moja yenye nguvu na ya kutoterereka katika karne ya 21.

 

Euro ina faida mbalimbali na faida hizo zinaweza zikaonwa na kuhisiwa katika ngazi tofauti, kwa mtu mmoja mmoja na kwa biashara na baadae uchumi mzima kwa ujumla.

 

Faida hizi za euro zinajumuisha:

•    Bidhaa nyingi na bei tulivu kwa wateja na wananchi kwa ujumla

•    Ulinzi mzuri zaidi na fursa nyingi zaidi kwa biashara na masoko

•    Kuboresha uimara na ukuaji wa uchumi

•    Kuongeza ushirikiano baina ya masoko ya fedha

•    Uwepo mkubwa zaidi wa umoja wa ulaya katika uchumi wa dunia

•    Ishara inayoonesha umoja wa ulaya Faida hizi nyingi zina uhusiano.

 

Kwa mfano, Utulivu wa uchumi ni mzuri kwa nchi husika kwasababu inawezesha serikali kufanya mipango ya baadae kwa umakini na ufanisi zaidi. Vivyo hivyo utulivu wa kiuchumi unafaidisha biashara kwasababu inapunguza kutokuwa na uhakika hivyo makampuni yanawekeza zaidi. Hivyo, hata wananchi wanafaidika kwasababu kunakuwa na ajira nyingi zaidi na kazi nzuri na zenye uhakika zaidi.        

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon