Kiwanda cha mbolea chajengwa Mtwara

August 12, 2016

Alisema kiwanda cha mbolea kinachotarajiwa kujengwa, kitahitaji gesi kiasi cha futi za ujazo trilioni 0.8 kwa kipindi cha miaka 20 na kusisitiza kuwa serikali imejipanga katika kuhakikisha kuwa gesi ya kutosha inazalishwa ili kuendana na mahitaji ya kiwanda hicho pamoja na matumizi mengine ya majumbani.Akielezea uwezo wa kampuni zilizopo Mtwara katika uzalishaji wa gesi ya kutosha, Profesa Ntwalikwa alifafanua kuwa, kampuni ya Ndovu Resources Limited iliyopo katika eneo la Ntorya ipo katika programu ya kuchimba visima ambapo imeshachimba kisima kimoja ambacho kimeweza kutoa kiasi cha futi za ujazo trilioni 0.15.Eneo la hekta 400 latengwa. Serikali kwa kushirikiana na kampuni ya Helm kutoka Ujerumani inatarajia kujenga kiwanda kikubwa cha mbolea katika eneo la Msanga Mkuu mkoani Mtwara. 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa Justin Ntalikwa (kushoto) akisalimiana na Meneja Uendeshaji wa Mnazi Bay, David Chaudronnier (kulia) mara baada ya kuwasili katika kituo hicho

 

 

Hayo yalielezwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa Justin Ntalikwa katika nyakati  tofauti katika ziara ya siku  tatu mkoani Mtwara ya kutembelea maeneo ambayo gesi inazalishwa na kujiridhisha iwapo itatosha katika uendeshaji wa kiwanda kikubwa cha mbolea kinachotarajiwa kujengwa.

Profesa Ntalikwa alisema kuwa kutokana na ugunduzi wa gesi nyingi mkoani Mtwara  wawekezaji wengi wameanza kuonesha nia ya kuwekeza katika mkoa  huo hususan katika uanzishwaji wa viwanda vya mbolea na saruji.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Kamishna Msaidizi wa Madini- Kanda ya Kusini, Mhandisi Benjamin Mchwampaka (kushoto) akiwasilisha taarifa ya maendeleo ya sekta ya madini katika kanda hivyo kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa Justin Ntalikwa (kulia) mara Profesa Ntalikwa alipofanya ziara katika kituo hicho.

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon