Kikwete ahimiza Afrika Kuwekeza Sekta ya Elimu

Rais mstaafu wa Tanzania Jakaya Kikwete aliyeongoza awamu yake ya nne alisema Afrika itaendelea kubaki nyuma kama hawataweka mbinu na jitihada za msingi katika sekta ya elimu.

Kauli hiyo aliito tarehe 24 Septemba jijini New York katika tamasha la Global Citizen katika viwanja vya Central Park.

Tamasha hilo ambalo hufanyika kila mwaka huwaleta pamoja viongozi wa sekta mbalimbali,wanaharakati na idadi kubwa ya watu wanaounga mkono jitihada hizo. Fedha zinazopatikana katika tamasha hilo husaidia kutekeleza yale waliyojadili. Kikwete ambaye pia ni kamishna katika kamisheni ya kimataifa kuhusu elimu alitaka wanaharakati na viongozi wa afrika kuafanya jitihada za makusudi ili kusaidia vizazi vya afrika kupata maendeleo katika upande wa elimu. Alisema ……… ‘’Afrika yangu, itakuwa makazi ya vijana bilioni moja ififkapo mwaka 2050, na tayari ipo hatua ya nyuma kabisa kielimu. Kama hatutawawezesha vijana hao kwa kuwapatia ujuzi na maarifa, uchumi wa afrika utashuka sana na watoto wengi hawataweza kufika mashuleni ifikapo mwaka 2030 kutokana na hamna maelimisho hayo kwa sasa’’. Katika harakati hizo tamasha hilo lilimtangaza Rihanna mwanamuziki wa kimarekani kuwa balozi wa elimu kupitia taasisi yake ya Clara Lionel na hana budi kufanya kampeni ili kuhakikisha watoto wote wa kiume na wa kike wanapata elimu.

#economy #history #war

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu